naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term Exam 2025 · Question 15

Mwandishi ametumia maneno hayo yote ili kuonyesha adabu. Ni lipi ambalo halionyeshi adabu?

From Kiswahili — Midterm Assessment 2025 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Shule ya msini, Manufaa,
S.L.P 4200-00200,
MAMBOLEO.
24-02-2024

Kwa rafiki mpendwa, Wami,
Pokea salamu nyingi kutoka kwangu, nikitumai u mzima kama kigongo. Mimi pia ni mzima. Namshukuru Mungu kunijalia afya njema. Je, huko shuleni kwenu unaendeleaje?
Lengo kuu la kukuandikia waraka huu ni kukualika katika siku ya kupeana zawadi shuleni mwetu. Sherehe hii itafanyika tarehe 19 Aprili mwaka huu.
Tafadhali nakuomba usikose kuhudhuria. Mimi nitakuwa miongoni kwa wale watakaotuzwa siku hiyo kwani, niliibuka wa kwanza katika mtihani wa kati ya muhula.
Nakuomba uje na wazazi wako na marafiki zetu wote. Asante na ninakutakia kila la heri katika yote ufanyayo. Endelea kutia bidii masomoni kwani bidii hulipa. Kwaheri.
Mimi rafiki yako mpendwa,
Jitihada Mbula.

15. Mwandishi ametumia maneno hayo yote ili kuonyesha adabu. Ni lipi ambalo halionyeshi adabu?

  1. AAsante
  2. BLengo
  3. CNakuomba
  4. DTafadhali.

Answer

B. Lengo

"Lengo" si neno la adabu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test