CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term Exam 2025 · Question 12
Barua ya aina hii huitwa barua
From Kiswahili — Midterm Assessment 2025 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Shule ya msini, Manufaa,
S.L.P 4200-00200,
MAMBOLEO.
24-02-2024
Kwa rafiki mpendwa, Wami,
Pokea salamu nyingi kutoka kwangu, nikitumai u mzima kama kigongo. Mimi pia ni mzima. Namshukuru Mungu kunijalia afya njema. Je, huko shuleni kwenu unaendeleaje?
Lengo kuu la kukuandikia waraka huu ni kukualika katika siku ya kupeana zawadi shuleni mwetu. Sherehe hii itafanyika tarehe 19 Aprili mwaka huu.
Tafadhali nakuomba usikose kuhudhuria. Mimi nitakuwa miongoni kwa wale watakaotuzwa siku hiyo kwani, niliibuka wa kwanza katika mtihani wa kati ya muhula.
Nakuomba uje na wazazi wako na marafiki zetu wote. Asante na ninakutakia kila la heri katika yote ufanyayo. Endelea kutia bidii masomoni kwani bidii hulipa. Kwaheri.
Mimi rafiki yako mpendwa,
Jitihada Mbula.
12. Barua ya aina hii huitwa barua
- Aya kirafiki
- Brasmi
- Cya kiofisi
- Dpepe
Answer
A. ya kirafiki
Ameandikiwa rafiki.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- “...mzima kama kigongo” ni fani gani ya lugha?Question 13
- Chagua sentensi ambayo ni sahihi kulingana na kifungu.Question 14
- Mwandishi ametumia maneno hayo yote ili kuonyesha adabu. Ni lipi ambalo halionyeshi adabu?Question 15
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo 18.Question 18