CBC Grade 5 Kiswahili Mid Term Exam 2025 · Question 9
Ni jukumu la nani kukomesha ufisadi?
From Kiswahili — Midterm Assessment 2025 (Set 14) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ufisadi umekuwa janga kubwa katika nchi yetu ya Kenya. Katika miji mikubwa, midogo au vijijini ufisadi umekuwa jambo la kawaida. Watu hushiriki ufisadi kwa sababu mbalimbali kama vile kupata huduma mbalimbali, kupata kazi, bidhaa bandia kutoka sehemu moja jadi nyingine.
Nchi ya Kenya hupoteza pesa nyingi sana kila mwaka kutokana na ufisadi. Kwa sababu hii, huduma zinazofaa kuwafikia wananchi haziwezi kama vile: barabara kujengwa, elimu bora, kujenga hospitali na kupata maji safi.
Jambo hili hivi sasa limetufika kooni na hatuwezi kulinyamazia kamwe. Ni lazima tusimame imara kupiga vita dhidi ya ufisadi. Hili ni jukumu langu na lako. Naomba kila mmoja wetu tushirikiane ili tufaulu katika vita dhidi ya ufisadi.
9. Ni jukumu la nani kukomesha ufisadi?
- AMimi
- BWewe
- CKila mwananchi
- DAskari
Answer
C. Kila mwananchi
"Hili ni jukumu langu na lako."
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni methali ipi inaweza kutumika kueleza ujumbe katika aya ya mwisho?Question 10
- Mwandishi wa barua hii anaitwaje?Question 11
- Barua ya aina hii huitwa baruaQuestion 12
- “...mzima kama kigongo” ni fani gani ya lugha?Question 13
- Chagua sentensi ambayo ni sahihi kulingana na kifungu.Question 14
- Mwandishi ametumia maneno hayo yote ili kuonyesha adabu. Ni lipi ambalo halionyeshi adabu?Question 15