CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 13
Kwa nini msimulizi anasema likizo yake ya Disemba ilikuwa ya kufurahisha?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Likizo ya Disemba ilikuwa nzuri sana. Ninaikumbuka hadi sasa. Tulikuwa tumeahidiwa kuzuru mbuga ya wanyama ili kujionea ndege wa porini na wanyama wengine wa mwituni. Usiku kabla ya safari, nilizipanga nguo zangu vizuri. Nililala usingizi wa mang'amung'amu nikingoja asubuhi ifike. Asubuhi na mapema wazazi wangu walinipatia maagizo. Wakanipa pesa za matumizi na chakula cha kutosha kisha nikaelekea shuleni kwa matarajio makuu. Shule yetu ilikodi basi ambalo lingebeba wanafunzi wa gredi yetu ya tano, safari yetu ya kuelekea Bondeni ilianza saa mbili kamili. Njiani, mandhari yalikuwa ya kuvutia sana. Tuliingia mbugani baada ya kulipa kiingilio. Nilifurahia kuwaona kanga, mwewe na tai. Ndege hao walinipendeza sana. Alasiri, tulirudi nyumbani, tulienda moja kwa moja hadi hotelini. Tukala, tukapumzika na kuanza rasmi safari ya kurejea nyumbani. Wengi wetu tulikuwa na bashasha kwa kuwa ilikuwa mara yetu ya kwanza kuzuru mbuga hiyo.
13. Kwa nini msimulizi anasema likizo yake ya Disemba ilikuwa ya kufurahisha?
- AKwa sababu bado anaikumbuka.
- BKwa sababu alitembelea mbuga ya wanyama.
- CKwa sababu alisafiri pamoja na wenzake.
- DKwa sababu likizo ilikuwa ndefu.
Answer
B. Kwa sababu alitembelea mbuga ya wanyama.
Ziara ya mbugani.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini msimulizi alipata usingizi wa mang'amung'amu usiku kabla ya safari?Question 14
- Katika kifungu, neno "bashasha" lina maana gani?Question 15
- Chagua jibu sahihi la pengo la 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la pengo la 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la pengo la 18.Question 18
- Chagua jibu sahihi la pengo la 19.Question 19