naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 15

Katika kifungu, neno "bashasha" lina maana gani?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Likizo ya Disemba ilikuwa nzuri sana. Ninaikumbuka hadi sasa. Tulikuwa tumeahidiwa kuzuru mbuga ya wanyama ili kujionea ndege wa porini na wanyama wengine wa mwituni. Usiku kabla ya safari, nilizipanga nguo zangu vizuri. Nililala usingizi wa mang'amung'amu nikingoja asubuhi ifike. Asubuhi na mapema wazazi wangu walinipatia maagizo. Wakanipa pesa za matumizi na chakula cha kutosha kisha nikaelekea shuleni kwa matarajio makuu. Shule yetu ilikodi basi ambalo lingebeba wanafunzi wa gredi yetu ya tano, safari yetu ya kuelekea Bondeni ilianza saa mbili kamili. Njiani, mandhari yalikuwa ya kuvutia sana. Tuliingia mbugani baada ya kulipa kiingilio. Nilifurahia kuwaona kanga, mwewe na tai. Ndege hao walinipendeza sana. Alasiri, tulirudi nyumbani, tulienda moja kwa moja hadi hotelini. Tukala, tukapumzika na kuanza rasmi safari ya kurejea nyumbani. Wengi wetu tulikuwa na bashasha kwa kuwa ilikuwa mara yetu ya kwanza kuzuru mbuga hiyo.

15. Katika kifungu, neno "bashasha" lina maana gani?

  1. AHuzuni
  2. BMshangao
  3. CMatumaini
  4. DFuraha

Answer

D. Furaha

Bashasha ni furaha.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test