naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 12

Katika kifungu, neno "siha" lina maana gani?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Baadhi ya itikadi za kidini na za kijamii zimechangia ukiukaji wa haki za watoto. Mtoto azaliwapo, ana haki ya kupewa lishe bora. Sharti alishwe aina zote za vyakula hasa protini, kabohaidreti au wanga, vitamini na madini. Vyakula vya protini ni aina zote za nyama na nafaka za jamii ya maharagwe. Vyakula hivi huwezesha mtoto kukua na kuwa na siha nzuri. Hata hivyo anapokosa vyakula vya protini, hufifia na kushambuliwa na ugonjwa wa kwashakoo. Vyakula vya wanga huongeza nguvu mwilini. Baadhi ya vyakula hivi ni chapati, ugali, uji na hata mkate. Vitamini huimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Matunda na mboga hasa ndivyo huwa na vitamini kwa wingi. Mbali na lishe bora, mtoto pia ana haki ya kuvishwa mavazi bora. Mavazi kuukuu humwaibisha mtoto mbele ya watu na wenzake. Vile vile, watoto wana haki ya kuishi katika makazi bora na yaliyo safi ili kumwepusha kuambukizwa magonjwa. Elimu ni muhimu katika maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo itikadi zinazopuuza elimu zinapaswa kupigwa marufuku. Elimu ni haki ya kimsingi ya kila mtoto.

12. Katika kifungu, neno "siha" lina maana gani?

  1. AMaisha
  2. BAfya
  3. CTabia
  4. DMwenendo

Answer

B. Afya

Siha ni afya.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test