CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 10
Nyama, maharagwe na mayai ni vyakula vya aina gani?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Baadhi ya itikadi za kidini na za kijamii zimechangia ukiukaji wa haki za watoto. Mtoto azaliwapo, ana haki ya kupewa lishe bora. Sharti alishwe aina zote za vyakula hasa protini, kabohaidreti au wanga, vitamini na madini. Vyakula vya protini ni aina zote za nyama na nafaka za jamii ya maharagwe. Vyakula hivi huwezesha mtoto kukua na kuwa na siha nzuri. Hata hivyo anapokosa vyakula vya protini, hufifia na kushambuliwa na ugonjwa wa kwashakoo. Vyakula vya wanga huongeza nguvu mwilini. Baadhi ya vyakula hivi ni chapati, ugali, uji na hata mkate. Vitamini huimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Matunda na mboga hasa ndivyo huwa na vitamini kwa wingi. Mbali na lishe bora, mtoto pia ana haki ya kuvishwa mavazi bora. Mavazi kuukuu humwaibisha mtoto mbele ya watu na wenzake. Vile vile, watoto wana haki ya kuishi katika makazi bora na yaliyo safi ili kumwepusha kuambukizwa magonjwa. Elimu ni muhimu katika maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo itikadi zinazopuuza elimu zinapaswa kupigwa marufuku. Elimu ni haki ya kimsingi ya kila mtoto.
10. Nyama, maharagwe na mayai ni vyakula vya aina gani?
- AHuongeza nguvu mwilini.
- BHuimarisha kinga ya mwili.
- CHujenga na kukuza mwili.
- DHumnenepesha mtu.
Answer
C. Hujenga na kukuza mwili.
Vyakula vya protini hujenga mwili.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na kifungu, ni haki ngapi za watoto zilizotajwa?Question 11
- Katika kifungu, neno "siha" lina maana gani?Question 12
- Kwa nini msimulizi anasema likizo yake ya Disemba ilikuwa ya kufurahisha?Question 13
- Kwa nini msimulizi alipata usingizi wa mang'amung'amu usiku kabla ya safari?Question 14
- Katika kifungu, neno "bashasha" lina maana gani?Question 15
- Chagua jibu sahihi la pengo la 16.Question 16