CBC Grade 5 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 8
Mgeni akiwa na tabia isiyopendeza, wenyeji walifanya nini?
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 12) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Ukarimu ni jambo linalohusudiwa na takribani Waafrika wote. Hapo zamani, ilikuwa vigumu kumwona Mwafrika akila kabla hajajua hali ya jirani yake na kumpelekea kile kizuri alichopika. Kinyume na baadhi ya watu wa siku hizi wanaotawaliwa na uchoyo pamoja na uroho. Ukarimu wa Mwafrika ulionekana zaidi hasa alipotembelewa na mgeni. Makaribisho aliyoyapata, tabasamu zisizokwisha, maneno matamu matamu, mazungumzo murua ni baadhi ya mambo yaliyofunua moyo wa mgeni. Katika jamii nyingi, mgeni alichinjiwa mbuzi, kondoo, ng'ombe au hata ngamia siku yake ya kwanza kama ishara na dalili ya furaha yao kwa kufika kwake. Watu husema mgeni njoo mwenyeji apone. Mgeni ni baraka wala si balaa. Sio mzigo kamwe. Awe ni wa kuleta ujumbe au kujulia jamaa hali, masuala ya mgeni hupewa kipaumbele. Hata ikiwa mgeni ni thakili wenyeji wake hujaribu kila mbinu ili kutuliza moyo wake. Wenyeji humdekeza hadi ugeni uishe. Hatimaye hataondoka mikono mitupu. Mkononi hatakosa zawadi. Wanaporejea makwao huzuni hutanda na baadhi ya watu hujikuta machozi yakiwadondoka hasa ikiwa mgeni alikuwa karimu na mwenye nidhamu.
8. Mgeni akiwa na tabia isiyopendeza, wenyeji walifanya nini?
- AWalimvumilia.
- BWalimkwepa.
- CWalimfukuza.
- DHawakumfurahia.
Answer
A. Walimvumilia.
Hata mgeni thakili, wenyeji walijaribu kutuliza moyo wake.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini mgeni alichinjiwa mnyama siku ya kwanza alipowasili?Question 9
- Nyama, maharagwe na mayai ni vyakula vya aina gani?Question 10
- Kulingana na kifungu, ni haki ngapi za watoto zilizotajwa?Question 11
- Katika kifungu, neno "siha" lina maana gani?Question 12
- Kwa nini msimulizi anasema likizo yake ya Disemba ilikuwa ya kufurahisha?Question 13
- Kwa nini msimulizi alipata usingizi wa mang'amung'amu usiku kabla ya safari?Question 14