CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 11
Ni nini kingefanyika iwapo msimulizi angekosa kupika chakula kitamu?
From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Nakumbuka vyema Krismasi ya mwaka uliopita. Mama alituandalia sherehe ya kukata na shoka. Kila mmoja wetu nyumbani alipewa majukumu mbalimbali. Mimi nilipewa la upishi. Nani asiyejua upishi wangu? Hata wewe unaufahamu.
Siku moja mama alimwalika Juma ampikie pilau. Huu ni wakati mama alikuwa ametembelewa na wageni. Nilimtazama Juma alivyotumia vifaa vya kupikia, njia za kupika na viungo vya kupikia pilau.
Juma alikuwa mpishi hodari. Hii ilitokana na uzoefu wake wa aina mbalimbali za upishi wa pilau na chapati kwa kitoweo cha nyama.
Nilipokea jukumu alilonipa mama kwa bashasha, nikaahidi kufanya kila niwezalo kumfurahisha. Niliandaa pilau tamu mno. Harufu ya pilau hiyo ilienea kote.
Wazazi, ndugu na wageni walioalikwa walifurahia pilau hiyo. Walikula wakamaliza fyu! Walishiba baada ya kuongeza bilauri mbili za sharubati. Watu wote walikula shibe yao. Majirani walikula chakula chote walichopelekewa na mama. Mama alinibandika jina “mpishi bora.” Ama kweli chanda chema huvikwa pete.
Baada ya sherehe, mimi na ndugu zangu tulishirikiana kuosha vyombo. Tulivipanga vyombo hivyo vizuri kwenye rafu.
11. Ni nini kingefanyika iwapo msimulizi angekosa kupika chakula kitamu?
Answer
Wageni hawangefurahia
Chakula kibaya hakifurahiwi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Methali, chanda chema huvikwa pete katika kifungu inaeleza nini kuhusu msimulizi?Question 12
- Je, Zubeda alienda katika ofisi ya mwalimu wakati gani?Question 13
- Zubeda ni mtoto mwaminifu kwa kuwa?Question 14
- Unafikiri ni kwa nini ni makosa kusoma barua za watu wengine?Question 15
- Taja neno lingine lenye maana sawa na barua.Question 16
- Mti huu una nomino zifuatazo: furaha, uzi, hekima, ukarimu, werevu. Chagua nomino ambayo si ya dhahania kwenye mti huu:Question 17