CBC Grade 5 Kiswahili Mock Exam 2025 · Question 15
Kichwa kipi chafaa habari hii?
From Kiswahili — First Trial Assessment 2025 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 11-15.
Ningependa kuishi mji wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina sehemu mbili: mji wa Kale na mji Mpya. Watu waliokuja kutoka sehemu mbalimbali za Asia, Bara Hindi na Uarabuni wote waliishi mji huu. Majumba mengi ya Mji wa Kale yanafanana na majumba ya Uarabuni, Bara Hindi na Uingereza. Watu wanatoka sehemu mbalimbali za dunia kuja kustarehe katika mji huu. Ninapenda historia ya Mombasa. Pia, watu wengi ni Waislamu kama familia yangu. Pia, ninapenda kukutana na watu tofauti. Hata hivyo, ningependa kuishi mji mpya kwa sababu usafiri ni rahisi, bei yake si ghali.
Ninapenda mji mpya zaidi ya mji wa Kale kwa sababu mji wa Kale ni wa familia ya kirafiki. Kwa mfano, Mombasa ina hoteli za kifahari. Hii ni muhimu kwa sababu familia yangu na rafiki yangu wataweza kuja ziara na kukaa hoteli karibu nami. Pia, kuna maduka makubwa kama duka kuu, sinema na shule nzuri sana. Hii ni muhimu kwa sababu ninaweza kwenda dukani kisha niende kwenye sinema baadaye.
15. Kichwa kipi chafaa habari hii?
- ASherehe za Mombasa.
- BMombasa mji wetu.
- CMji ningetamani kuishi.
- DZiara yangu Mombasa.
Answer
C. Mji ningetamani kuishi.
Mwandishi anaanza "Ningependa kuishi mji wa Mombasa".
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu sahihi la pengo 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la pengo 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la pengo 18.Question 18
- Chagua jibu sahihi la pengo 19.Question 19
- Chagua jibu sahihi la pengo 20.Question 20
- Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo. Kamilisha salamu. U hali gani?Question 21