CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6
Kulingana na sentensi ya pili, marafiki waliotajwa ni wangapi?
From Kiswahili — Revision Paper 5 (2026) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 6 hadi 9.
Hapo zamani za kale paliondokea marafiki ambao walipendana kama chanda na pete. Walishirikiana kwa kila jambo. Marafiki hawa walikuwa nyati, kifaru, ndovu na kobe. Marafiki hawa hawakutaka kutenganishwa. Japo sungura alitaka wakosane, walikuwa na upendo wa dhati.
Siku moja sungura alitumia ujanja wake ili wakosane. Kila walipofanya kazi, siku iliyofuata walikuta kazi yao imeharibiwa kuna siku walipanda miche pamoja. Walipokuja siku iliyofuata, walikuta imeng'olewa. Walizozana sana kwa kuwa hakuna mnyama hata mmoja alikaribia shamba lao. Kobe alitumia busara yake ili kujua aliyekuwa akiuharibu urafiki wao. Alitengeneza mtego wa nyavu. Marafiki zake hawakujua alikuwa ametengeneza mtego.
6. Kulingana na sentensi ya pili, marafiki waliotajwa ni wangapi?
- AWawili
- BWatatu
- CWanne
- DWatano
Answer
C. Wanne
Marafiki ni nyati, kifaru, ndovu na kobe: wanne.