CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1
Wagonjwa walingoja daktari wakiwa wapi?
From Kiswahili — Revision Paper 5 (2026) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Ni zahanatini pambajioni pamejaa wagonjwa wanaosubiri zamu yao kutibiwa. Daktari anamkaribisha mgonjwa chumbani na kumwashiria kuketi kitini.)
Daktari: Karibu sana na ninakuombea afueni ya haraka.
Mgonjwa: Asante sana daktari. Hujambo?
Daktari: Sijambo. Una tatizo gani?
Mgonjwa: Nina maumivu ya tumboni. Niliaanza kuumwa jana jioni.
Daktari: Una shida nyingine.
Mgonjwa: Ndio. Nilitapika mara moja leo asubuhi.
Daktari: Pole utapona.
Mgonjwa: Nashukuru.
Daktari: Naomba nikupime joto la mwili. Tafadhali vua sweta nikupime. (Baada ya muda mfupi) Naona joto liko juu kidogo. Dawa nitakazokupatia zitakusaidia.
Mgonjwa: Asante tabibu.
Daktari: Nimeshatuma maelezo ya dawa kwa mhudumu wa duka la dawa kupitia intaneti. Nenda kule atakupa. Utapona. Kwaheri.
Mgonjwa: Asante daktari.
1. Wagonjwa walingoja daktari wakiwa wapi?
- AZahanatini
- BPambajioni
- CNje
- DHospitalini
Answer
B. Pambajioni
Mazungumzo yanaanza: "Ni zahanatini pambajioni pamejaa wagonjwa wanaosubiri zamu yao." Wagonjwa walisubiri pambajioni.