CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4
Jogoo aliyeibiwa alikuwa wa nani?
From Kiswahili — Revision Paper 4 (2026) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo haya kati ya Mwema na Gakuo kisha ujibu maswali 1 hadi 5
MADA: TABIA NZURI NI NGAO
Gakuo na Mwema wamekutana barabarani kila mtu akielekea zake. (Gakuo amebeba gunia lenye vitu na Mwema amebeba jembe)
Mwema: Shikamoo Gakuo.
Gakuo: z z z
Mwema: Natoka shambani kulima. Je, waelekea wapi jioni?
Gakuo: Naelekea kanisani kusali.
Mwema: Ala! Kanisa lipi saa hii? Umebeba nini kwenye gunia?
Gakuo: Uko na maswali mengi, kwani wewe ni polisi? Nimebeba vitabu vya Bibilia (mara jogoo anawika kutoka kwa gunia)
Mwema: Ala! Mbona unadanganya. Hebu nivione. Huyu sio yule jogoo wa jirani yangu aliyeibiwa leo usiku. Wacha nipigie polisi. (Gakuo anatimua mbio na kupotea)

4. Jogoo aliyeibiwa alikuwa wa nani?
- AWa jirani wa Mwema
- BWa polisi
- CWa jirani wa Gakuo
- DWa Mwema
Answer
A. Wa jirani wa Mwema
Mwema anasema, "Huyu sio yule jogoo wa jirani yangu aliyeibiwa leo usiku." Jogoo alikuwa wa jirani wa Mwema.