CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 3 · Question 1
Ni Salamu gani hutumika wakati wa kuamkua mtu asubuhi?
From Kiswahili — TISMA Exams 007 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mwalimu: Hodi! Wanafunzi wangu, habari zenu?
Wanafunzi: Karibu mwalimu, tuko salama.
Mwalimu: Mko vipi leo?
Wanafunzi: Tu wazima, mwalimu! Tuna furaha kuwa na wewe.
Mwalimu: Leo tutaongea kuhusu maamkuzi na maagano katika jamii yetu. Je, watu huamkuana vipi?
Wanafunzi: Watu huamkuana kwa kusema, "Habari ya asubuhi". au "U hali gani?"
Mwalimu: Hiyo ni nzuri. Je, kuna aina nyingine ya maamkuzi?
Wanafunzi: "Alamsiki" au "Siku njema" Pia ni salamu tunazotumia.
Mwalimu: Hivyo ndivyo ilivyo. Na wakati wa kuagana ni maneno gani tunayotumia?
Wanafunzi: Tunatumia "Kwaheri", "tutaonana" au "lala salama".
Mwalimu: Maagano haya ni muhimu sana kwa uhusiano wetu na wengine.
Wanafunzi: Asante, Mwalimu! Tutatumia maamkuzi haya kila wakati.
Ni Salamu gani hutumika wakati wa kuamkua mtu asubuhi?
- ALala salama
- BTutaonana
- CHabari ya asubuhi.
- DU hali gani?
Answer
C. Habari ya asubuhi.
Wanafunzi walisema watu huamkuana kwa kusema "Habari ya asubuhi". Salamu hii hutajwa asubuhi tu.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni gani kati ya maneno haya hutumika kuagana?Question 2
- Pendo alimwambia mzazi wake "Alamsiki" Je, mzazi alijibu kwa kusema vipi?Question 3
- Neno lipi hutumika kutoa shukrani kwa mtu akikufanyia jambo zuri?Question 4
- Ni nini umuhimu wa maamkuzi na maagano?Question 5
- Ni nini kilichomfanya Zuhura kuwa na huzuni?Question 6
- Mashindano ya mitindo ya mavazi yalifanyika wapi?Question 7