CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 3 · Question 5
Ni nini umuhimu wa maamkuzi na maagano?
From Kiswahili — TISMA Exams 007 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Mwalimu: Hodi! Wanafunzi wangu, habari zenu?
Wanafunzi: Karibu mwalimu, tuko salama.
Mwalimu: Mko vipi leo?
Wanafunzi: Tu wazima, mwalimu! Tuna furaha kuwa na wewe.
Mwalimu: Leo tutaongea kuhusu maamkuzi na maagano katika jamii yetu. Je, watu huamkuana vipi?
Wanafunzi: Watu huamkuana kwa kusema, "Habari ya asubuhi". au "U hali gani?"
Mwalimu: Hiyo ni nzuri. Je, kuna aina nyingine ya maamkuzi?
Wanafunzi: "Alamsiki" au "Siku njema" Pia ni salamu tunazotumia.
Mwalimu: Hivyo ndivyo ilivyo. Na wakati wa kuagana ni maneno gani tunayotumia?
Wanafunzi: Tunatumia "Kwaheri", "tutaonana" au "lala salama".
Mwalimu: Maagano haya ni muhimu sana kwa uhusiano wetu na wengine.
Wanafunzi: Asante, Mwalimu! Tutatumia maamkuzi haya kila wakati.
Ni nini umuhimu wa maamkuzi na maagano?
- AKuonyesha upendo tu.
- BKufanya kazi kwa haraka.
- CKusikia sauti za wengine.
- DKuonyesha heshima na kujali.
Answer
D. Kuonyesha heshima na kujali.
Mwalimu alisema maagano ni muhimu kwa uhusiano wetu na wengine — tunaonyesha heshima na kuwajali wenzetu. Jibu A lina neno "tu", kwa hivyo halijakamilika.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni nini kilichomfanya Zuhura kuwa na huzuni?Question 6
- Mashindano ya mitindo ya mavazi yalifanyika wapi?Question 7
- Zuhura aliishi katika kijiji kilichoitwaje?Question 8
- Zuhura alishinda mashindano kwa sababu gani?Question 9
- Hadithi hii inatufundisha nini?Question 10
- Kamusi hutueleza yote yafuatayo isipokuwaQuestion 11