CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 3
Eleza maana ya methali "Chema chajiuza."
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Sarufi na Matumizi ya Lugha, Methali
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–5.
Mteja: Umeshindaje kaka? Naona una mboga zinazovutia sana. Bei ya fungu hili ni gani?
Muuzaji: Niko vyema mwenzangu. Hizi nimezivuna leo kutoka shambani mwangu. Tazama nyanya, pilipili, vitunguu na karoti.
Mteja: Hehehe! Leo wateja watakuja wengi. Naomba mafungu mawili ya sukumawiki.
Muuzaji: Samahani dada, fungu moja la sukumawiki ni shilingi ishirini.
Mteja: Chema chajiuza. Nipe pia fungu moja la nyanya na vitunguu maji.
Muuzaji: Je, hutaki karoti leo?
Mteja: La, bado ninazo. Nilinunua nyingi jana. Vyote ni shilingi ngapi?
Muuzaji: Vyote ni shilingi themanini.
Mteja: Nitalipa kwa simu.
Muuzaji: Asante sana dada.
Mteja: Kwaheri kaka.
Eleza maana ya methali "Chema chajiuza."
Answer
Kitu kizuri hakihitaji kutangazwa; ubora wake huwavutia wanunuzi chenyewe.
"Chema chajiuza" maana yake kitu kizuri hakihitaji kutangazwa wala kusifiwa sana; watu hukiona na kukinunua kwa sababu ya ubora wake. Mteja aliitumia kwa sababu mboga za muuzaji zilikuwa zinavutia sana, hivyo zingenunuliwa haraka.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini mteja hakununua karoti?Question 4
- Ni tukio gani linaonyesha matumizi ya teknolojia katika mazungumzo haya?Question 5
- Kwa nini Sungura alijulikana sana katika kijiji?Question 6
- Sungura alipiga mswaki wakati gani?Question 7
- Sungura alinawa mikono lini?Question 8
- Usafi una faida gani kwa afya ya mtu?Question 9