CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 6
Kwa nini Sungura alijulikana sana katika kijiji?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–10.
Sungura alifahamika sana katika kijiji chao. Umaarufu wake ulitokana na jinsi alivyothamini na kupenda usafi. Alikuwa mfano wa kuigwa na wanakijiji wote kwa sababu kila mara alionekana akiwa amevaa nguo safi na zilizopigwa pasi vizuri. Hakuwa akila chakula chochote bila kunawa mikono kwanza. Aidha, alihakikisha kuwa amenawa mikono kwa sabuni na maji safi kila inapohitajika. Kila siku alipiga mswaki asubuhi na jioni bila kukosa. Kwa sababu ya kuzingatia usafi huo, Sungura alikuwa na afya njema wakati wote.
Kwa nini Sungura alijulikana sana katika kijiji?
Answer
Kwa sababu alithamini na kupenda usafi.
Kifungu kinasema: "Umaarufu wake ulitokana na jinsi alivyothamini na kupenda usafi." Alivaa nguo safi zilizopigwa pasi na alinawa mikono kila mara.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Sungura alipiga mswaki wakati gani?Question 7
- Sungura alinawa mikono lini?Question 8
- Usafi una faida gani kwa afya ya mtu?Question 9
- Sungura alikuwa mfano bora kwa nani katika kijiji?Question 10
- Wafula na rafiki yake walikuwa wakienda wapi?Question 11
- Kwa nini dereva aliendesha gari kwa tahadhari?Question 12