CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 5
Ni tukio gani linaonyesha matumizi ya teknolojia katika mazungumzo haya?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–5.
Mteja: Umeshindaje kaka? Naona una mboga zinazovutia sana. Bei ya fungu hili ni gani?
Muuzaji: Niko vyema mwenzangu. Hizi nimezivuna leo kutoka shambani mwangu. Tazama nyanya, pilipili, vitunguu na karoti.
Mteja: Hehehe! Leo wateja watakuja wengi. Naomba mafungu mawili ya sukumawiki.
Muuzaji: Samahani dada, fungu moja la sukumawiki ni shilingi ishirini.
Mteja: Chema chajiuza. Nipe pia fungu moja la nyanya na vitunguu maji.
Muuzaji: Je, hutaki karoti leo?
Mteja: La, bado ninazo. Nilinunua nyingi jana. Vyote ni shilingi ngapi?
Muuzaji: Vyote ni shilingi themanini.
Mteja: Nitalipa kwa simu.
Muuzaji: Asante sana dada.
Mteja: Kwaheri kaka.
Ni tukio gani linaonyesha matumizi ya teknolojia katika mazungumzo haya?
Answer
Mteja alisema atalipa kwa simu.
Mwishoni mteja alisema, "Nitalipa kwa simu." Kulipa pesa kwa kutumia simu ni matumizi ya teknolojia.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Kwa nini Sungura alijulikana sana katika kijiji?Question 6
- Sungura alipiga mswaki wakati gani?Question 7
- Sungura alinawa mikono lini?Question 8
- Usafi una faida gani kwa afya ya mtu?Question 9
- Sungura alikuwa mfano bora kwa nani katika kijiji?Question 10
- Wafula na rafiki yake walikuwa wakienda wapi?Question 11