naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 10

Sungura alikuwa mfano bora kwa nani katika kijiji?

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6–10.

Sungura alifahamika sana katika kijiji chao. Umaarufu wake ulitokana na jinsi alivyothamini na kupenda usafi. Alikuwa mfano wa kuigwa na wanakijiji wote kwa sababu kila mara alionekana akiwa amevaa nguo safi na zilizopigwa pasi vizuri. Hakuwa akila chakula chochote bila kunawa mikono kwanza. Aidha, alihakikisha kuwa amenawa mikono kwa sabuni na maji safi kila inapohitajika. Kila siku alipiga mswaki asubuhi na jioni bila kukosa. Kwa sababu ya kuzingatia usafi huo, Sungura alikuwa na afya njema wakati wote.

Sungura alikuwa mfano bora kwa nani katika kijiji?

Answer

Kwa wanakijiji wote.

Kifungu kinasema Sungura "alikuwa mfano wa kuigwa na wanakijiji wote".

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test