CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 13
Walipofika Nakuru walikula nini?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 11–15.
Wafula na rafiki yake walitoka mjini Mumias mapema asubuhi kuelekea Nairobi. Walikuwa wakienda kumtembelea mjomba wa Wafula ambaye alikuwa akifanya kazi katika mji huo. Walifika kwenye stani ya magari saa kumi na mbili asubuhi, na safari yao ilianza saa moja kamili. Dereva wao aliendesha gari kwa tahadhari ili kuepuka ajali.
Walipofika mjini Nakuru, walipata nafasi ya kujinunulia chamcha. Baada ya kula, walikunywa maji safi kisha wakarudi garini. Hatimaye, waliwasili Nairobi saa moja za jioni, wakikuta mjomba wao amewasubiri kwenye stani ya magari.
Walipofika Nakuru walikula nini?
Answer
Walikula chamcha.
Walipofika Nakuru "walipata nafasi ya kujinunulia chamcha". Chamcha ni chakula cha mchana.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Walimpata mjomba wao wapi walipofika Nairobi?Question 14
- Walikuwa wanaenda kumtembelea nani?Question 15
- Mama Rehema alienda ___(16)___ kununua nyama.Question 16
- ___(17)___ aliweka mkoba wake chini katika buchari.Question 17
- ...aliweka mkoba wake chini katika ___(18)___.Question 18
- Alijiunga na wanunuzi wengine ili apimiwe nyama kwa ___(19)___.Question 19