naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Opener Exam Term 2 2026 · Question 2

Muuzaji huyu anaweza pia kuwa nani?

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2026 Set 8 (Lugha) · 2 marks · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1–5.

Mteja: Umeshindaje kaka? Naona una mboga zinazovutia sana. Bei ya fungu hili ni gani?
Muuzaji: Niko vyema mwenzangu. Hizi nimezivuna leo kutoka shambani mwangu. Tazama nyanya, pilipili, vitunguu na karoti.
Mteja: Hehehe! Leo wateja watakuja wengi. Naomba mafungu mawili ya sukumawiki.
Muuzaji: Samahani dada, fungu moja la sukumawiki ni shilingi ishirini.
Mteja: Chema chajiuza. Nipe pia fungu moja la nyanya na vitunguu maji.
Muuzaji: Je, hutaki karoti leo?
Mteja: La, bado ninazo. Nilinunua nyingi jana. Vyote ni shilingi ngapi?
Muuzaji: Vyote ni shilingi themanini.
Mteja: Nitalipa kwa simu.
Muuzaji: Asante sana dada.
Mteja: Kwaheri kaka.

Muuzaji huyu anaweza pia kuwa nani?

Answer

Anaweza kuwa mkulima kwa sababu alivuna mboga hizo kutoka shambani mwake.

Muuzaji alisema, "Hizi nimezivuna leo kutoka shambani mwangu." Mtu anayelima na kuvuna mboga shambani ni mkulima. Pia ni mfanyabiashara kwa sababu anauza mboga hizo sokoni.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test