naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 12

Ndovu alimnunulia nyanya yake zawadi gani?

From Kiswahili — CBC Assessment 2025 Set 1 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali 11 - 15.

Hapo zamani za kale, palikuwa na marafiki wawili. Marafiki hao walikuwa Ndovu na Mbogo. Marafiki hao walipendana sana. Walishirikiana katika shughuli zao za kila siku. Siku moja, Ndovu alipanga safari ya kumtembelea nyanya yake kijiji jirani. Ndovu alikwenda sokoni na kumnunulia nyanya yake zawadi. Zawadi hiyo ilikuwa ni dagaa na jamvi. Mbogo naye alimchumia maembe ili ampelekee nyanya yake kama zawadi. Siku ya safari, marafiki hao waliamka mapema. Walisaidiana na kuweka vitu kwenye motokaa. Mbogo alilazimika kubaki ili kulinda mazao yao yasiharibiwe na Tumbili. Ndovu alipofika kijijini, alipata nyanya yake amepika ubwabwa na mboga za majani. Ndovu na nyanya yake waliketi juu ya jamvi na kula pamoja. Ilipofika jioni Ndovu alifunga safari kurudi kijijini kwao. Nyanya alimpa zawadi ya peremende. Ndovu alifurahi sana.

13. Ndovu alimnunulia nyanya yake zawadi gani?

  1. AMaembe
  2. BDagaa
  3. CShuka
  4. DNguo.

Answer

B. Dagaa

Ndovu alinunua dagaa na jamvi sokoni. Maembe yalichumwa na Mbogo, hayakununuliwa na Ndovu.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test