CBC Grade 4 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 11
Ndovu alipanga safari ya kuelekea wapi?
From Kiswahili — CBC Assessment 2025 Set 1 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali 11 - 15.
Hapo zamani za kale, palikuwa na marafiki wawili. Marafiki hao walikuwa Ndovu na Mbogo. Marafiki hao walipendana sana. Walishirikiana katika shughuli zao za kila siku. Siku moja, Ndovu alipanga safari ya kumtembelea nyanya yake kijiji jirani. Ndovu alikwenda sokoni na kumnunulia nyanya yake zawadi. Zawadi hiyo ilikuwa ni dagaa na jamvi. Mbogo naye alimchumia maembe ili ampelekee nyanya yake kama zawadi. Siku ya safari, marafiki hao waliamka mapema. Walisaidiana na kuweka vitu kwenye motokaa. Mbogo alilazimika kubaki ili kulinda mazao yao yasiharibiwe na Tumbili. Ndovu alipofika kijijini, alipata nyanya yake amepika ubwabwa na mboga za majani. Ndovu na nyanya yake waliketi juu ya jamvi na kula pamoja. Ilipofika jioni Ndovu alifunga safari kurudi kijijini kwao. Nyanya alimpa zawadi ya peremende. Ndovu alifurahi sana.
12. Ndovu alipanga safari ya kuelekea wapi?
- AKumtembelea nyanya yake.
- BKumwona mama yake.
- CKumtembelea rafiki yake.
- DKuenda sokoni kuchuma maembe.
Answer
A. Kumtembelea nyanya yake.
Kisa kinasema Ndovu "alipanga safari ya kumtembelea nyanya yake kijiji jirani".