CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2
Ni kweli kusema kuwa
From Kiswahili — Revision Paper 1 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.
(Ni sokoni, Teya anapita sokoni akitoka kazini)
Teya: Umeshindaje? Naona unazo mboga zinazovutia kwelikweli. Bei gani fungu hili?
Mwuzaji: Vyema sana mwenzangu. Hizi nimezivuna kutoka shambani mwangu leo. Pia kuna nyanya, pilipili, vitunguu na karoti. Leo, siku zote bei hutegemea mapatano.
Teya: Hahaha! Leo wateja wote watapitia hapa kibandani pako. Haya naomba uniuzie mafungu mawili ya sukumawiki na....
Mwuzaji: Samahani dada. Natumai unajua bei ya mwaka huu mpya. Fungu moja la sukumawiki sasa ni shilingi ishirini.
Teya: Gharama ya maisha nayo! Niuzie mafungu mawili ya sukumawiki, fungu moja la nyanya na vitunguu fungu moja.
Mwuzaji: Karoti leo?
Teya: Bado zipo. Nilinunua nyingi. Vyote ni shilingi ngapi?
Mwuzaji: Naam, vyote ni shilingi themanini.
Teya: Shika noti ya mia moja unipe salio.
Ni kweli kusema kuwa
- AMwuzaji alikuwa na shamba
- BTeya aliuza bidhaa sokoni
- CTeya na Mwuzaji walikuwa maadui
- DMwuzaji alikuwa shambani
Answer
A. Mwuzaji alikuwa na shamba
Mwuzaji anasema: "Hizi nimezivuna kutoka shambani mwangu leo." Kwa hivyo alikuwa na shamba. Teya ndiye aliyenunua, na walizungumza kwa urafiki sokoni.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni bidhaa gani ilinunuliwa na Teya na huwa tunda?Question 3
- Teya alitumia pesa ngapi kununua bidhaa?Question 4
- Mwuzaji alifaa kumpa Teya pesa ngapi?Question 5
- Ni nini maana ya nahau amekula chumvi nyingi?Question 6
- Mzee Busara alikuwa na sifa gani kuu?Question 7
- Ni nani walihadithiwa kulingana na kifungu hiki?Question 8