naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 8

Mtu anaposema "salalee" huwa

From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati

Soma kifungu kinachofuata kisha ujibu maswali 6 hadi 9.

Ulikuwa wakati wa mapumziko tukicheza mpira uwanjani. Mimi na rafiki zangu tulikuwa tukicheza kandanda. Ghalfa, Naftali aliupiga mpira kwa nguvu zake zote akitaka kufunga bao. Mpira ulipaa angani kama ndege na kuingia kwenye msitu uliokuwa karibu na shule.

Sote tuliingiwa na wasiwasi. Nani atauendea mpira? Tulisimama huku tukiwaza nini cha kufanya. Mara Muturi akaamua kuruka ua na kwenda kuuleta mpira. Alikuwa kijana jasiri kama simba. Aliruka na kuingia msituni kwenda kuuleta mpira huku sisi tukiwa tunamtazama kwa hofu.

"Njooni muone!" Tulisikia sauti yake ikiita. Mimi sikutaka kwenda kabisa. Nilidhani alikuwa ameona nyoka.

"Ni nini?" Tonje alikuwa ameshafika. Moyo wangu ulikuwa mikononi.

Mara tukasikia sauti ya vifaranga na kuku. Salalee! Kumbe kuku ambaye alikuwa amepotea shuleni kwa muda wa wiki tatu alikuwa amepotelea katika msitu huo. Humo, alikuwa ametaga mayai na hata akaangua vifaranga.

Tulikimbia shuleni na kumwita mwalimu wetu wa darasa Bwana Chebai ambaye tulishirikiana naye kuwashika vifaranga hao pamoja na kuku na kuwarudisha shuleni. Karibu tuusahau mpira wetu uliokuwa karibu na kuku huko msituni.

Mtu anaposema "salalee" huwa

  1. AAmeshangaa
  2. BAmeogopa
  3. CAmekasirika
  4. DAmefurahia

Answer

A. Ameshangaa

"Salalee!" ni neno la kuonyesha mshangao.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test