CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 12
Sungura alimwambia mama yake ajifiche wapi kulingana na kifungu hiki?
From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Hapo zamani za kale, sungura na fisi waliishi pamoja kama ndugu wa tumbo moja. Walipendana sana. Walifanya mambo yao pamoja. Siri za sungura alizificha fisi, naye sungura akamfichia fisi siri zake. Walipendana kama ulimi na mate.
Siku moja sungura alimraukia fisi akiwa na wazo la kushangaza. Alimwambia fisi wakawauze mama zao. Fisi alishangaa. Sungura alisema kuwa siku hizi mama zao hawapiki chakula kitamu tena. Isitoshe, wamezeeka na hawana faida kama zamani. Fisi alifikiria kwa muda kisha akakubaliana na sungura. Alisema kuwa kesho wakutane asubuhi kuwauza mama zao sokoni.
Sungura alikimbia nyumbani kwa furaha. Alimwambia mama yake ajifiche chini ya kitanda. Alichukua mgomba wa ndizi na kuuweka kwenye gunia. Asubuhi fisi alifika na mama yake akiwa amemweka ndani ya gunia. Alikuwa amempiga kama ngoma hadi akazirai ili asimsumbue wakienda sokoni.
Njiani walikubaliana kuwa pesa watakazozipata watanunua nyama, chipsi na vyakula vingine vitamu ambavyo mama zao hawakujua jinsi ya kuvipika. Fisi alimuuza mama yake huku sungura aliuza mgomba wa ndizi. Jioni waliporudi nyumbani, fisi alibaki peke yake huku njaa ikimvamia kwani hakuwa na mtu wa kumpikia. Sungura naye alipikiwa na mama yake aliyekuwa nyumbani.
Siku moja fisi alikuja kumtembelea sungura akamkosa. Alipobisha mlangoni mara kadhaa alishangaa kumwona mama yake sungura akiwa ndani. Aligundua kuwa sungura alikuwa amemhadaa. Tangu siku hiyo, urafiki wao ulivunjikia hapo.
Sungura alimwambia mama yake ajifiche wapi kulingana na kifungu hiki?
- AJuu ya nyumba
- BNdani ya pazia
- CChini ya kitanda
- DJuu ya kitanda
Answer
C. Chini ya kitanda
Kifungu kinasema, "Alimwambia mama yake ajifiche chini ya kitanda."
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni mwanafunzi gani hakununua njugu?Question 13
- Ni kwa nini Omari hakununua peremende kwa mujibu wa kifungu hiki?Question 14
- Ni mwanafunzi yupi ambaye hakupanda pikipiki?Question 15
- Chagua jibu sahihi la nafasi ya 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la nafasi ya 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la nafasi ya 18.Question 18