CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Ni mwanafunzi yupi ambaye hakupanda pikipiki?
From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Wanafunzi wanne walienda sokoni kununua bidhaa. Omari, Jumbe na Tito walinunua maembe, njugu, mayai na ndizi. Nadia alinunua bidhaa kama za watatu hao ila hakununua njugu. Walipokuwa wakitembea sokoni, waliona peremende. Wote walinunua peremende lakini Omari akakataa kwa sababu mwalimu wake alikuwa amewakataza kula vitu vya sukari ambavyo vinaweza kuharibu meno. Alinunua mswaki mpya. Wote walirudi nyumbani kwa kutumia pikipiki isipokuwa Tito ambaye alitembea kwa sababu kwao si mbali na sokoni.
Ni mwanafunzi yupi ambaye hakupanda pikipiki?
- ATito
- BOmari
- CJumbe
- DNadia
Answer
A. Tito
"Wote walirudi nyumbani kwa kutumia pikipiki isipokuwa Tito ambaye alitembea."