naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11

Sungura alienda kwa fisi na wazo la kushangaza wakati gani kulingana na kifungu hiki?

From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.

Hapo zamani za kale, sungura na fisi waliishi pamoja kama ndugu wa tumbo moja. Walipendana sana. Walifanya mambo yao pamoja. Siri za sungura alizificha fisi, naye sungura akamfichia fisi siri zake. Walipendana kama ulimi na mate.

Siku moja sungura alimraukia fisi akiwa na wazo la kushangaza. Alimwambia fisi wakawauze mama zao. Fisi alishangaa. Sungura alisema kuwa siku hizi mama zao hawapiki chakula kitamu tena. Isitoshe, wamezeeka na hawana faida kama zamani. Fisi alifikiria kwa muda kisha akakubaliana na sungura. Alisema kuwa kesho wakutane asubuhi kuwauza mama zao sokoni.

Sungura alikimbia nyumbani kwa furaha. Alimwambia mama yake ajifiche chini ya kitanda. Alichukua mgomba wa ndizi na kuuweka kwenye gunia. Asubuhi fisi alifika na mama yake akiwa amemweka ndani ya gunia. Alikuwa amempiga kama ngoma hadi akazirai ili asimsumbue wakienda sokoni.

Njiani walikubaliana kuwa pesa watakazozipata watanunua nyama, chipsi na vyakula vingine vitamu ambavyo mama zao hawakujua jinsi ya kuvipika. Fisi alimuuza mama yake huku sungura aliuza mgomba wa ndizi. Jioni waliporudi nyumbani, fisi alibaki peke yake huku njaa ikimvamia kwani hakuwa na mtu wa kumpikia. Sungura naye alipikiwa na mama yake aliyekuwa nyumbani.

Siku moja fisi alikuja kumtembelea sungura akamkosa. Alipobisha mlangoni mara kadhaa alishangaa kumwona mama yake sungura akiwa ndani. Aligundua kuwa sungura alikuwa amemhadaa. Tangu siku hiyo, urafiki wao ulivunjikia hapo.

Sungura alienda kwa fisi na wazo la kushangaza wakati gani kulingana na kifungu hiki?

  1. AAsubuhi
  2. BJioni
  3. CAlasiri
  4. DAdhuhuri

Answer

A. Asubuhi

"Sungura alimraukia fisi": kuraukia ni kwenda kwa mtu asubuhi na mapema.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test