naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7

Muturi aliposema 'njooni muone' alikuwa ameona nini?

From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu

Soma kifungu kinachofuata kisha ujibu maswali 6 hadi 9.

Ulikuwa wakati wa mapumziko tukicheza mpira uwanjani. Mimi na rafiki zangu tulikuwa tukicheza kandanda. Ghalfa, Naftali aliupiga mpira kwa nguvu zake zote akitaka kufunga bao. Mpira ulipaa angani kama ndege na kuingia kwenye msitu uliokuwa karibu na shule.

Sote tuliingiwa na wasiwasi. Nani atauendea mpira? Tulisimama huku tukiwaza nini cha kufanya. Mara Muturi akaamua kuruka ua na kwenda kuuleta mpira. Alikuwa kijana jasiri kama simba. Aliruka na kuingia msituni kwenda kuuleta mpira huku sisi tukiwa tunamtazama kwa hofu.

"Njooni muone!" Tulisikia sauti yake ikiita. Mimi sikutaka kwenda kabisa. Nilidhani alikuwa ameona nyoka.

"Ni nini?" Tonje alikuwa ameshafika. Moyo wangu ulikuwa mikononi.

Mara tukasikia sauti ya vifaranga na kuku. Salalee! Kumbe kuku ambaye alikuwa amepotea shuleni kwa muda wa wiki tatu alikuwa amepotelea katika msitu huo. Humo, alikuwa ametaga mayai na hata akaangua vifaranga.

Tulikimbia shuleni na kumwita mwalimu wetu wa darasa Bwana Chebai ambaye tulishirikiana naye kuwashika vifaranga hao pamoja na kuku na kuwarudisha shuleni. Karibu tuusahau mpira wetu uliokuwa karibu na kuku huko msituni.

Muturi aliposema 'njooni muone' alikuwa ameona nini?

  1. AMwili wa binadamu
  2. BNyoka wa kutisha
  3. CKuku na vifaranga
  4. DMpira wao

Answer

C. Kuku na vifaranga

Baadaye walisikia sauti ya vifaranga na kuku: Muturi alikuwa amempata kuku aliyepotea pamoja na vifaranga wake.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test