CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 2
Ni neno gani ambalo linaweza kupatikana katika kadi ya maneno ya heshima na adabu?
From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 5.
(Darasani. Ni asubuhi na mwalimu wa Kiswahili Bw. Galacha anaingia na madaftari akiwa na tabasamu)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi? (huku anaweka madaftari mezani na kuandika tarehe ubaoni)
Wanafunzi: Hatujambo mwalimu hali gani?
Mwalimu: Njema sana. Asanteni. Mnaweza kukaa chini.
Wanafunzi: (huku wakiketi chini kwa utulivu) Shukran mwalimu.
Mwalimu: Leo hii tutajifunza kuhusu salamu na maneno ya adabu. (anawatazama wanafunzi). Naomba wanafunzi wawili wajitolee kuja hapa mbele kuigiza salamu. (anatoa kadi zenye maneno ya adabu na heshima)
Sigi: Mimi mwalimu! (anainua mkono wake. Mwalimu anamwashiria aende mbele)
Mwalimu: Mpigieni makofi kwa kujitolea. (darasa linapiga makofi) Mwengine?
Jeremi: (Anatimka mbio kuelekea mbele ya darasa bila kuzungumza kisha anaanza kucheka).
Mwalimu: Vizuri Jeremi, lakini unafaa kujieleza kwa heshima. Kila mwana mwema sharti adumishe heshima wakati wote.
Ni neno gani ambalo linaweza kupatikana katika kadi ya maneno ya heshima na adabu?
- ANjoo
- BSema
- CLakini
- DSamahani
Answer
D. Samahani
"Samahani" ni neno la adabu tunalotumia kuomba msamaha au kuomba jambo kwa heshima.
More Grade 4 Kiswahili questions from this test
- Ni mwanafunzi yupi hakuonyesha heshima na nidhamu katika mazungumzo haya?Question 3
- Mwalimu alimwelekeza Jeremi kuwa.Question 4
- Taja jambo moja ambalo mwalimu Galacha hakulifanya alipoingia darasani.Question 5
- Kulingana na kifungu hiki, wanafunzi walikuwa wanafanya nini uwanjani?Question 6
- Muturi aliposema 'njooni muone' alikuwa ameona nini?Question 7
- Mtu anaposema "salalee" huwaQuestion 8