naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4

Mwalimu alimwelekeza Jeremi kuwa.

From Kiswahili — Revision Paper 2 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 5.

(Darasani. Ni asubuhi na mwalimu wa Kiswahili Bw. Galacha anaingia na madaftari akiwa na tabasamu)

Mwalimu: Hamjambo wanafunzi? (huku anaweka madaftari mezani na kuandika tarehe ubaoni)
Wanafunzi: Hatujambo mwalimu hali gani?
Mwalimu: Njema sana. Asanteni. Mnaweza kukaa chini.
Wanafunzi: (huku wakiketi chini kwa utulivu) Shukran mwalimu.
Mwalimu: Leo hii tutajifunza kuhusu salamu na maneno ya adabu. (anawatazama wanafunzi). Naomba wanafunzi wawili wajitolee kuja hapa mbele kuigiza salamu. (anatoa kadi zenye maneno ya adabu na heshima)
Sigi: Mimi mwalimu! (anainua mkono wake. Mwalimu anamwashiria aende mbele)
Mwalimu: Mpigieni makofi kwa kujitolea. (darasa linapiga makofi) Mwengine?
Jeremi: (Anatimka mbio kuelekea mbele ya darasa bila kuzungumza kisha anaanza kucheka).
Mwalimu: Vizuri Jeremi, lakini unafaa kujieleza kwa heshima. Kila mwana mwema sharti adumishe heshima wakati wote.

Mwalimu alimwelekeza Jeremi kuwa.

  1. AKila mwana mwema lazima aadhibiwe akikosa heshima
  2. BKila mwana mwema lazima adumishe tabia njema wakati wote
  3. CKila mwana mwema lazima aende mbele ya darasa
  4. DKila mwana mwema lazima asiitikie mwalimu akimwita.

Answer

B. Kila mwana mwema lazima adumishe tabia njema wakati wote

Mwalimu alisema, "Kila mwana mwema sharti adumishe heshima wakati wote." Hii ndiyo tabia njema.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test