CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 35
Mmea ni nini?
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yote.
Mmea ni kiumbe kilicho na uhai chenye majani, mizizi na shina. Mimea inaweza kupandwa kwa mbegu au kwa kutumia matawi. Faida za mimea ni nyingi na hazipaswi kupuuzwa.
Baadhi ya mimea huzalisha matunda ambayo huliwa na binadamu, wanyama na ndege. Mimea mingine huliwa mashina kama vile miwa. Mingine huliwa mizizi kama vile viazi, na mingine huliwa matunda kama vile maembe.
Mimea mingi huwa na rangi ya kijani kibichi.
Mmea ni nini?
Answer
Mmea ni kiumbe kilicho na uhai chenye majani, mizizi na shina.
Sentensi ya kwanza ya kifungu inaeleza: "Mmea ni kiumbe kilicho na uhai chenye majani, mizizi na shina."
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.