naQonda

CBC Grade 3 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 6

SEHEMU YA 2: KUSOMA KWA SAUTI Soma hadithi hii kwa sauti.

From Kiswahili — Term 3 Opener Exams 2026 · 10 marks · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Sauti

Jamii ni watu wanaoishi pamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali. Wema hutengeneza jamii bora. Ni vizuri kufahamu jinsi ya kuishi vizuri na wanajamii wengine. Ili kuishi vizuri na wanajamii wengine unapaswa kujipenda, kujitambua na kuwapenda wengine. Kujipenda ni kujidhamini na kujikubali. Mtoto anayejipenda anatunza afya yake. Vilevile, anaepuka matendo mabaya na anakuwa na tabia njema wakati wote. Mtoto mwema huwa baraka kwa wazazi wake na jamii. Mara nyingi mtoto mwema huwatii wakubwa wake. Akitumwa huenda bila kukasirika. Wanafunzi wengi wamefunzwa wema na adabu shuleni. Inawapasa kutumia mafunzo hayo kila mahali. Walimu na wazazi pia wanapaswa kuwa vielelezo bora katika jamii. Jamii bora watu huwa wema.

SEHEMU YA 2: KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi hii kwa sauti.

Answer

Jamii ni watu wanaoishi pamoja na kushirikiana katika shughuli mbalimbali. Wema hutengeneza jamii bora. Ni vizuri kufahamu jinsi ya kuishi vizuri na wanajamii wengine. Ili kuishi vizuri na wanajamii wengine unapaswa kujipenda, kujitambua na kuwapenda wengine. Kujipenda ni kujidhamini na kujikubali. Mtoto anayejipenda anatunza afya yake. Vilevile, anaepuka matendo mabaya na anakuwa na tabia njema wakati wote. Mtoto mwema huwa baraka kwa wazazi wake na jamii. Mara nyingi mtoto mwema huwatii wakubwa wake. Akitumwa huenda bila kukasirika. Wanafunzi wengi wamefunzwa wema na adabu shuleni.…

Soma kila neno wazi na usimame kwenye kitone.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 3 Kiswahili questions from this test