CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 5
Mi hapa natangazia, kila mmoja sikia, Siku hizi twangamia, kutofuata sheria, Barabarani twalia, kupoteza familia, Tuzingatie kanuni, za barabara tuishi.…
From Test 102 — Revision 6 Kiswahili Karatasi 2 · 5 marks · Topic: Fasihi, Ushairi
Mi hapa natangazia, kila mmoja sikia,
Siku hizi twangamia, kutofuata sheria,
Barabarani twalia, kupoteza familia,
Tuzingatie kanuni, za barabara tuishi.
Madereva macho kuwa, kila wakati sukani,
Taratibu mtakuwa, endesheni mitaani,
Hata mtakapokuwa, vilevile mashambani,
Tuzingatie kanuni, za barabara tuishi.
Abiria wanaboda, hata nasi tusikie,
Tahadhari ni ibada, baadaye furahie,
Wazazi kaka na dada, salama tuwafikie,
Tuzingatie kanuni, za barabara tuishi.
a)
Eleza ujumbe wa shairi hili.
(Ala. 2)
Fafanua dhamira ya shairi hili?
b)
(Ala. 1)
Shairi hili lina beti ngapi?
c)
(Ala. 1)
Arudhi ni sheria au kanuni zinazofuatwa katika utunzi wa mashairi.
d)
Taja aina ya
shairi hili.
(Ala. 1)
Answer
Maudhui ni uzingativu wa sheria za barabara. Shairi linaelimisha watu wawe makini wanapotumia barabara. Lina beti tatu na ni shairi la tarbia.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- (Insha na Utangulizi wa Fasihi) Jina Nambari ya usajili Shule Tarehe Maagizo: Karatasi hii ina sehemu mbili na B.…Question 1
- SEHEMU B: (Alama 35) ZOEZI LA 11: FASIH! SIMULIZI (Alama10) 2. Soma taqrifa ifuqtayo kishq ujibu maswali. Hapo zamani…Question 2
- "Vipi Boss? Uliweza kukitazama kile kinyang'anyiro cha soka cha saa nne usiku? Mimi sikuweza. Mvua ya ghafla…Question 3
- d) Fafanua sifa za wahusika uliotaja. (Al. 2) e) Kwa kutoa mfano, eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.…Question 4