naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 4

Mabula: Si utani mwenzangu. (Kimya) Baada.ya kufikiria sana nimeona kuwa lisilo budi hutendwa. Heri nikusaidie kukitafuta hicho kidogo. Kama ni baa…

From Test 96 — Revision 1 Kiswahili Karatasi 2 · 10 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia

Mabula:
Si utani mwenzangu. (Kimya) Baada.ya kufikiria sana nimeona kuwa lisilo budi hutendwa.
Heri nikusaidie kukitafuta hicho kidogo. Kama ni baa nimekwenda, kama ni mikahawani
nimefika. Ahadi zote nilizopewa zimekuwa si kitu. Pana haj a gani kujisumbua sana?
Mishi:
Mabula, itakuwa taabu kwako kwenda shambani. Miaka mingapi hii tangu uuinamishe
mgongo shambani?
Mabula:
Mtu hujikuna ajipatapo mishi.
Mishi:
(Kwa huzuni) Ni kweli Mabula, lakini itakuwa vigumu zaidi kwetu kwenda shambani. Cheo
ulichokuwa nacho hakikuruhusu kufanya kazi ya aina hii. Mabula tutazificha wapi nyuso
zetu? Tutasemwa sana! Kwa vyovyote vile lazima tuufiche uchi wetu. Jina Iako ni kubwa.
Mabula:
Mishi, mtu hali •sifa. Hata sifa hizo ni zajana. Leo anachonidai ni tofauti na hiyojana.
Mishi:
Ni heri uende huko mikahawani kukutana na wenzako tuone iwapo ya heri itafunguka.
Mabula:
Nimechoka Mishi.
Mishi:
Gangaganga za mganga humwacha mgonjwa na matumaini.
12. Dondoo hili ni sehemu yatamthilia. Elezamaanayatamthilia ukirejelea dondoo hili. (alama 1)
13.
Taja maudhui yoyote mawili yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)
14.
Tambua sifa mojamoja ya wahusika wafuatao. (alama 2)
a) Mishi
b) Mabula
15.
Ploti ni mfuatano wa matukio katika kazi ya fasihi: Eleza ploti ya sehemu hii ya tamthilia. (alama 3)
Tambua sifa za tamthilia zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
16.

Answer

Tamthilia ni kipera cha fasihi andishi chenye muundo wa mazungumzo. Ni maskini mtaamushi. Wahusika ni Mishi, mwenye matumaini, na Mabula aliyetamauka. Ni wakati wa jioni. Mishi na Mabula wameamua kwenda shambani lakini Mishi anamkataza kwa kuwa atashusha hadhi yake. Tamthilia huwa na muundo wa mazungumzo, wahusika na huandikwa upande wa kushoto.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test