naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Revision Exam · Question 15

Unadhani ni nini kingetokea iwapo watu wangeendelea kukata miti na kutupa taka ovyo?

From Test 95 — Revision 1 Kiswahili Karatasi 1 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Kifungu cha Maswali 13–17
Kijiji cha Mpeketoni kilikuwa kidogo Iakini chenye miti iliyovutia hewa safi, kivuli na mvua. Kilikuwa
na mto uliotiririka maji safi. Udongo ulikuwa na rutuba hivi kwamba wanakijiji walinufaika sana kutokana
na zaraa. Kati ya wanakijiji, paliishi binti mmoja kwa jina Metina. Metina alikuwa msichana aliyependa
kusikiliza hadithi za babu yake zilizohusujinsi ya kutunza mazingira na maliasili.
Siku moja Metina aligundua kuwa wanakijiji walikuwa wakikata miti kiholela na mabiwi ya taka
yalitupwa popote. Udongo ulianza kukosa rutuba na mazao yakawa yanapungua siku baada ya siku.'Metina
alimuuliza babu yake, "mbona watu hawatunzi maliasili yetu tena?" "Watu hawajali tena mwanangu.
Wamesahau maliasili hutupa faida kadri tunavyoyatunza na kuyahifadhi" Baba alimjibu kwa sauti hafifu.
Metina alitamani sana kuleta mabadiliko. Aliwakusanya marafiki wake na majirani. Aliwashawishi
wapande miti kila sehemu iliyokuwa imekatwa miti kisha wanyunylzie maji na mbolea kwenye udongo ili
kurejesha rutuba.
Baada ya muda, kijiji cha Mpeketoni kilianza kubadilika na misitu ikamea tena. Mashamba yalipata
mazao tena na mto kuendelea kutiririka maji safi. Wanakijiji wote waligundua umuhimu wa kutunza maliasili.

Unadhani ni nini kingetokea iwapo watu wangeendelea kukata miti na kutupa taka ovyo?

  1. AMazao yangeendelea kudidimia kabisa.
  2. BMito ingeendelea kutiririsha maji.
  3. CWakazi wangefurahia hewa safi.
  4. DMvua ingeendelea kunyesha.

Answer

A. Mazao yangeendelea kudidimia kabisa.

The correct option is A.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test