CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 4
Soma hadithi hii kisha ujibu maswali. SEHEMU 1: ONYESHO 1I (Soiyan, binti wa miaka kumi na mmoja, anamsaidia mama yake katika shughuli za jikoni) Soiyan:…
From Test 93 — Kiswahili Karatasi 2 Muhula 2 Mei 2026 · 10 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia
Soma hadithi hii kisha ujibu maswali.
SEHEMU 1: ONYESHO 1I
(Soiyan, binti wa miaka kumi na mmoja, anamsaidia mama yake katika shughuli za jikoni)
Soiyan: Mama, baadhi ya mila katika jamii yangu zinanitia wasiwasi.
Mama: (Akimgeukia bintiye) Mila kama gani?
Soiyan: Mambo kama ukeketaji (Anatua kidogo) Nilisoma mtandaoni kuwa baadhi ya wasichana wanaopitia unyama huu huvuja damu hadi kufa.
Mama: Wajua jamaa zetu zimefuata utamaduni huo tangu jadi na jadudi. Wanaoenda kinyume wanaonekana kama 'outcasts'. Yaani wanatengwa na jamii.
Soiyan: Ni kweli kuwa mkataa wengi ni mchawi. Lakini haimaanishi tufuatane kama kondoo anavyomfuata mchinjaji akachinjwe.
Mama: Unayosema ni kweli binti yangu. Tazama, jamii yetu haina wanawake wengi walisoma. Hii ni kwa sababu wasichana wengi huozwa pindi tu wanapopashwa tohara.
Soiyan: Ninajua mambo yatabadilika.
Mama: (Akichanganyikiwa) Yatabadilika vipi ilhali wazee wetu wameshikilia Ki ki ki imani potovu ya kumdhalilisha mwanamke.
Soiyan: (Akionyesha furaha) Serikali imeweka sheria kali za kuwadhibiti wale wanaowaoza mabinti wadogo na wanaowanyanyasa kupitia ukeketaji. Wanaoendesha matendo yoyote ya dhuluma za kijinsia watatiwa mbaroni na kula kalenda.
Mama: Shabash! Hizo ni habari njema. Lau ningezaliwa enzi zenu hizo ningekuwa na bahati sana.
(wanaanza kuandika meza)
(a) Taja sifa mbili za tamthilia zinazojitokeza katika kifungu hiki. (Alama 2)
(b) Fafanua mifano miwili ya maudhui yasiyoshughulikiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)
(c) Eleza umuhimu wa maelekezo ya jukwaani katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)
(d) Jadili vipengele viwili vya lugha vinavyotumiwa katika onyesho hili. (Alama 2)
Answer
(a) Sifa mbili za tamthilia: i. Onyesho la mazungumzo kati ya wahusika. ii. Inaelezea mgogoro au changamoto za kijamii. (b) Maudhui yasiyoshughulikiwa: i. Ukeketaji na madhara yake kiafya. ii. Ukandamizaji wa wanawake kijamii. (c) Umuhimu wa maelekezo ya jukwaani: i. Kuonyesha mpangilio wa wahusika. ii. Kuonyesha hisia na matendo kwa usahihi. (d) Vipengele vya lugha: i. Methali au usemi wa mafumbo: “Ni kweli kuwa mkataa wengi ni mchawi.” ii. Mfanano / taswira: hisia na matukio yanayoelezwa kwa undani.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali Twashukuru na Jaladi, mkuu mwenye kibali, Asante kwa kutujali, kwa afya pia…Question 5
- Andika insha kwa kuendeleza mwanzo ufuatao: Endeleza kisa hiki hadi kukamilika. Nilipofika nyumbani siku hiyo jioni,…Question 1
- Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali. Nyani na Sokwe walikuwa wafugaji hodari. Mazizi yao yalishiba na kutapika…Question 2
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Zarika alikuwa mezani akifanya Hisabati. Alionekana akilaani huku akidai…Question 3