naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 2

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali. Nyani na Sokwe walikuwa wafugaji hodari. Mazizi yao yalishiba na kutapika mifugo ambao walizaana kila uchao. Siri…

From Test 93 — Kiswahili Karatasi 2 Muhula 2 Mei 2026 · 10 marks · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Nyani na Sokwe walikuwa wafugaji hodari. Mazizi yao yalishiba na kutapika mifugo ambao walizaana kila uchao. Siri ya ufanisi wao ilikuwa dhahiri. Wote walikuwa mchwa katika shughuli zao. Majirani zao waliwaonea gere lakini hakuna waliloweza kufanya kuzuia mafanikio ya marafiki hao waliopendana kama chanda na pete.
Siku moja, Nyani na Sokwe walifunga safari ya kuwapeleka baadhi ya mifugo wao sokoni wakauze. Walitaka kupata pesa za kukidhia aila zao mahitaji maadamu msimu wa krismasi ulikuwa unanukia. Makazi yao na sokoni palikuwa pua na mdomo. Kwa hivyo, haikuwachukua muda mrefu kufika.
Walianza shughuli za kupiga mnada mifugo wao. Wanunuzi walifika kwa wingi wakang’ang’ania kukutu mifugo ya Sokwe. Wengi hawakupata ujasiri wa kutupia macho mifugo wa Nyani waliokonda mithili ya ng’onda. Sokwe alipata kitita kikubwa cha pesa. Nyani, kwa upande wake alijawa na hasira za mkizi.
Mwishowe alikata shauri kuwauza mifugo wake kwa bei ya kutupa. Hata hivyo, wateja walinunua shingo upande.
Nyani alikuwa bubu katika safari ya kurudi nyumbani. Kimoyomoyo, aliona kuwa rafikiye Sokwe ni joka la mdimu kwanza ndiye aliyemzuia kufanikiwa katika uuzaji. Sokwe alitulia tuli akisubiri mambo yapoe kwanza.
Siku iliyofuata, baada ya moyo wa Nyani kutua kidogo, aliamua kumwendea sahibu yake aijue siri yake.
Alishuhudia namna wafanyakazi walivyosafisha vizimba vya kuku huku wakiwapa mifugo chanja na vyakula vyenye virutubisho.
“Elimu ni bahari, tulia nikufunze mambo ya ufugaji,” alisema Sokwe huku akimletea kalamu na karatasi ya kuandikia maelezo.
Nyani alitulia tuli akafunzwa kwa mapana na marefu kuhusu utunzaji wa wanyama.
(a) Hadithi hii ni ya aina gani? (Alama 1)
(b) Jadili sifa tatu za hadithi za aina hii. (Alama 3)
(c) Rafiki yako angependa kuwasilisha hadithi hii katika ukumbi wa shule. Taja vipengele vitatu vya uwasilishaji ambavyo utamshauri azingatie. (Alama 3)
(d) Eleza vipengele viwili vya lugha vilivyotumiwa katika hadithi hii. (Alama 2)
(e) Ni funzo lipi linalopatikana katika hadithi hii? (Alama 1)

Answer

(a) Aina ya hadithi: Hadithi ya wanyama / Fable. (b) Sifa tatu za hadithi ya aina hii: i. Inatumia wanyama kama wahusika wakuu. ii. Inafundisha funzo au maadili kwa msomaji. iii. Inaangazia tabia za wanyama kuakisi tabia za binadamu. (c) Vipengele vya uwasilishaji vya kuzingatia: i. Matamshi wazi na sauti inayofaa. ii. Hisia na hisi za wahusika kufahamika. iii. Mtiririko wa tukio ufuatwe bila kukosa muundo. (d) Vipengele vya lugha: i. Mfanano / Methali: “Elimu ni bahari.” ii. Onomatopoeia / taswira ya sauti: “pua na mdomo.” (e) Funzo: Elimu na maarifa ni muhimu katika kufanikisha shughuli.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test