naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 3

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Zarika alikuwa mezani akifanya Hisabati. Alionekana akilaani huku akidai kuwa Mwalimu Kombo alipenda kuwapa kazi…

From Test 93 — Kiswahili Karatasi 2 Muhula 2 Mei 2026 · 10 marks · Topic: Fasihi, Novela na Hadithi Fupi

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Zarika alikuwa mezani akifanya Hisabati. Alionekana akilaani huku akidai kuwa Mwalimu Kombo alipenda kuwapa kazi ngumu. “Anasema tusaidiwe na wazazi, mimi huwaona wazazi hao lini? Wakipiga mablanketi teke, wako njiani kuenda kazini. Tena wakati wakirudi sote tumeshalala fofofo! Nyumbani humu ninaishi kama yatima.”
Mawazo yake yalikatizwa na Sayora, kijakazi wao. Japo alikuwa mtumishi pale nyumbani. Umri wake ulimpita Zarika kwa miaka miwili tu. Sayora aliitupia macho kazi aliyokuwa akifanya Zarika. Kwake aliona rahisi kama papai kwa kijiko. Alianza kumwonyesha jinsi ya kufanya kazi hiyo. Zarika alishangaa ghaya ya kushangaa kwani Sayora alielezea vizuri kuliko mwalimu wao.
Zarika alishtuka. Awali, alidhani kuwa Sayora hakuwahi hata kuliona lango la shule. Alivyojua ni kuwa Sayora mwenyewe alikuwa yatima lakini hakujua zaidi ya hapo kuhusu maisha yake.
“Dada,” alisema Zarika kwa unyenyekevu, “hebu nieleze stori yako tafadhali. Huenda nikakusaidia.”
Maneno hayo yalimtonesha Sayora kidonda ambacho alidhani kimeanza kupona. Alikumbuka jinsi alivyokuwa wembe masomoni akiwa na matumaini ya kuishi vyema maishani. Hata hivyo, maisha yaliamua kumwonyesha shubiri. Gonjwa la Ukimwi lilikatiza ndoto zake lilipoamua kuwachukua wavyele wake.
(a) Taja mazingira yanayojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 1)
(b) Jadili masuala mawili ambayo mwandishi ameshughulikia katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)
(c) Jadili sifa moja ya Sayora inayojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 2)
(d) Huku ukitolea mifano mwafaka, jadili tamathali tatu za usemi zilizotumika katika sehemu hii ya novela. (Alama 3)

Answer

(a) Mazingi yanayojitokeza: Nyumba / mazingira ya nyumbani. Shule / mawasiliano ya kijamii. (b) Masuala mawili yaliyoshughulikiwa: i. Changamoto za kijamii na familia: wazazi wasiopatikana, maisha ya yatima. ii. Uelimishaji na usaidizi wa kijakazi mdogo: Sayora anamsaidia Zarika. (c) Sifa ya Sayora: Msaada na unyenyekevu; ana uwezo wa kufundisha na kusaidia wengine. (d) Tamathali za usemi: i. Methali / mfanano: “Rahisi kama papai kwa kijiko.” ii. Onomatopoeia: sauti ya kazi iliyoelezewa. iii. Taswira: maelezo ya hisia na hali za wahusika.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test