naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 1

Kwa nini Mawia anatamani kuwa rubani kulingana na mazungumzo?

From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Mazungumzo kati ya Chacha na Mawia
(Chacha anazungumza na rafiki yake Mawia.)
Chacha: Je, ungependa kufanya kazi gani baada ya kukamilisha masomo yako?
Mawia: Ningependa sana kuwa rubani. Marubani hulipwa mshahara mzuri sana na hawachoki kwa kufanya kazi ngumu. Je, wewe ungependelea kuwa nani?
Chacha: Ninatamani sana kuwa mkulima. Nalipenda sana somo la zaraa.
Mawia: (Akishangaa) Ala! Ukulima ni kazi kweli? Unataka kuishi ukiwa mchafu? Ukulima sio kazi nzuri hata kidogo.
Chacha: Kwa nini unasema si kazi nzuri?
Mawia: Kazi hiyo inachosha sana. Aidha, wakulima wengi ni maskini hohehahe.
Chacha: Hapo sikubaliani nawe kabisa, ndugu yangu. Ukulima ni kazi kama nyingine yoyote. Wapo wakulima wenye mali nyingi hata kuliko viongozi wakuu serikalini.
Mawia: (Akiwa na shauku) Enhee! Hebu nieleze zaidi, rafiki yangu.
Chacha: Mkulima mzuri huwekeza kwa kununua pembejeo za kilimo. Anaweza kununua mitambo ya kulima, kupalilia, kuvuna na hata kunyunyizia dawa. Sio lazima asagike kwenye mpini wa jembe kila siku.
Chacha: Si hayo tu, ukitumia mbinu za kisasa za kilimo, unaweza kujiongezea kipato kikubwa bila hata kuwa na shamba kubwa. Teknolojia mpya imechangia kuvumbuliwa kwa mbegu zinazostahimili ukame na vimelea. Kwa hivyo, mkulima huhakikishiwa mazao bora wakati wote.
Mawia: Kumbe! Nimekuwa na mtazamo tofauti sana kuhusu kilimo. Sasa umenifumbua macho. Sasa nakuunga mkono kikamilifu. Nimegundua kuwa una maarifa ya kutosha kuhusu kilimo.

Kwa nini Mawia anatamani kuwa rubani kulingana na mazungumzo?

  1. AIli asafiri kila mahali
  2. BAnaonelea kuwa kazi hiyo haichoshi
  3. CHajui kazi nyingine yoyote
  4. DMarubani ni watu wazuri kuliko wakulima

Answer

B. Anaonelea kuwa kazi hiyo haichoshi

Jibu sahihi ni B. Mawia anasema, "Marubani hulipwa mshahara mzuri sana na hawachoki kwa kufanya kazi ngumu." Kwa hiyo anatamani urubani kwa sababu anaona kazi hiyo haichoshi. Mawia hasemi kwamba anataka kusafiri kila mahali (A), kwamba hajui kazi nyingine (C), wala kwamba marubani ni watu wazuri kuliko wakulima (D); mambo hayo hayamo katika mazungumzo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test