CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 2
a) Taja wahusika wakuu wanne katika hadithi hii, mbali na Mzee Kobe. (alama 2)
From Test 85 — Kiswahili Paper 2 (KJSEA) · 2 marks · Topic: Fasihi, Fasihi Simulizi
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali kuanzia la 2(a) hadi 2(d).
Mzee Kobe alikuwa na shamba kubwa sana. Shambani mwake, alikuza mimea mbalimbali ikiwemo mboga, matunda na aina mbalimbali za mimea izaayo nafaka. Mbali na mimea hiyo, alikuwa ni mfugaji hodari wa kuku wa mayai. Mzee Kobe alikumbatia mbinu bora za kilimo na teknolojia iliyomsaidia kupata mazao bora na kwa wingi.
Majirani wa Mzee Kobe walikuwa ni Nyani, Ndovu, Swara na Paa. Wanyama hawa walijipakatia mikono tu; hawakujifunga masombo. Mara nyingi walikabiliwa na njaa maadamu hawakuwa na chochote cha kuvuna msimu wa kuvuna ulipowadia. Walipenda anasa na starehe, na walimkejeli Mzee Kobe alipokuwa akifanya kazi shambani kwa bidii. Kila msimu wa kuvuna, wanyama hao walipenda kumwibia Kobe mazao yake kutoka shambani. Hata hivyo, Kobe aliweka mitego kila mahali na wengi wao waliogopa kunaswa.
Wanyama hao hawakupendezwa na kitendo hicho cha Mzee Kobe kuwatega. Walilalamika na kumlaani kwa kuwauzia mazao kwa bei ya rejareja; walitaka awape bure bilashi. Hata hivyo, Kobe alipovuna mazao yake, aliacha kiasi fulani shambani na kisha kuitegua mitego aliyoweka. Wanyama walifurahia na kuyala mazao hayo kwa pupa.
Msimu mmoja, Mzee Kobe alisafiri ughaibuni na hivyo hakupanda chochote shambani mwake. Msimu wa mavuno ulipofika, wanyama walifika shambani kama kawaida yao ili kuona na kula walichoachiwa na Mzee Kobe. Kwa mshangao mkubwa, kwekwe na magugu tu ndio yaliyokuwa yamejaa shambani! Hawakuelewa kuwa baniani mbaya kiatu chake dawa. Waliyemwona adui, ndiye aliyekuwa msaada wao usiotajika. Aliporejea kutoka safarini, wanyama hao walimmininika nyumbani kwake, wakamwomba msamaha na kumshukuru kwa wema aliotenda bila wao kufahamu.

Answer
Wahusika wakuu ni Mzee Kobe, na majirani zake: Nyani, Ndovu, Swara na Paa.
Swali hili limebuniwa kufuatia muundo wa mwongozo rasmi wa kusahihisha, kwa kuwa hati asilia haikuchapisha maswali mahususi ya 2(a)-2(d) (pengo halisi kwenye hati asilia, lililoripotiwa kwa mtumiaji).
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- b) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika hadithi hii. (alama 3)Question 3
- c) Taja methali mbili zilizotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)Question 4
- d) Andika mafunzo matatu tunayoyapata kutokana na hadithi hii. (alama 3)Question 5
- a) Kazi za fasihi huwa na malengo maalum. Eleza dhamira kuu ya mwandishi katika sehemu hii ya novela. (alama 2)Question 6
- b) Eleza sifa mbili za mhusika (mnyaji) kwa mujibu wa dondoo hili la novela. (alama 2)Question 7
- c) Kwa kutoa mifano madhubuti, eleza mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (alama 3)Question 8