CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 6
a) Kazi za fasihi huwa na malengo maalum. Eleza dhamira kuu ya mwandishi katika sehemu hii ya novela. (alama 2)
From Test 85 — Kiswahili Paper 2 (KJSEA) · 2 marks · Topic: Fasihi, Novela na Hadithi Fupi
Soma dondoo lifuatalo la Novela ya 'Mshale wa Matumaini' (J. Habwe) kisha ujibu maswali.
Chakula kilikuwa kimepikwa vibaya vibaya. Hakikuwa na ladha yoyote. Nilikula tu kwa kuwa lisilo budi hutendwa. Niliungama kwamba siku zote mhitaji habagui.
Nililala usingizi wa pono usiku huo. Sikupinduka wala kuamka kwenda haja usiku kucha. Ninadhani hali ile ilitokana na uchovu mwingi niliokuwa nao usiku ule. Niliota nikiwa katika uwanja wa Ntaikuja nikiichezea kandanda timu yangu ya Nomads. Timu ya Nomads ilishindana na timu ya Ngorongoro mara kwa mara. Ngorongoro ilikuwa timu ya kijijini lakini ilikuwa hodari sana. Ilikuwa imeshinda timu nyingi mjini Madena. Ilishinda timu ya Lulu, timu ya Zawadi na timu ya Ngazija. Kwenye ndoto hiyo nilikuwa nikicheza nambari mbili. Katika kipindi cha kwanza, nilifunga bao la penalti. Nilitegemewa sana katika ulingo wa penalti. Kila mtu aliniamini. Baada ya dakika kadhaa nilifunga bao la pili. Tulicheza tukiwa na hakika ya ushindi.
Katika dakika kumi na tano za mwisho ndipo wachezaji wa timu ya Ngorongoro walipotuzaba mabao matatu mfululizo na kuibuka washindi. Kipindi kilipofika mwisho, tulitaka refa atupe muda zaidi lakini alikataa katakata. Hali ile iliibua fujo mle uwanjani. Wachezaji wa upande wetu walianza kumshambulia refa na hivyo ikawa fujo moja kwa moja. Wachezaji walikuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe.
Mchezaji mmoja alikuwa ameshika gogo kubwa na kuanza kunishambulia. Nilitoka shoti na kutoroka lakini hakukoma, akawa ananifukuza himahima. Nilimwomba anisamehe kwa kunyanyua mikono yangu juu lakini hakunielewa. Aliponikaribia alikuwa tayari kunipasua kichwa. Hapo nilipiga ukemi mkubwa.
Ghafla niliamka! Dah! Nilishtuka nilipojiona katika ulimwengu halisi badala ya ulimwengu wa kutisha wa ndotoni.

Answer
Dhamira kuu ni matumaini — jinsi ndoto ya msimulizi inavyoakisi changamoto za maisha halisi na hali ya kutafuta matumaini katikati ya mateso.
Angalia jibu la mfano na vigezo vya alama hapo juu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- b) Eleza sifa mbili za mhusika (mnyaji) kwa mujibu wa dondoo hili la novela. (alama 2)Question 7
- c) Kwa kutoa mifano madhubuti, eleza mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika sehemu hii ya novela. (alama 3)Question 8
- d) Maudhui ni masuala makuu yanayoshughulikiwa katika kazi ya fasihi. Fafanua masuala (maudhui) mawili…Question 9
- e) Eleza mandhari inayojitokeza (ya ndotoni au halisi) katika dondoo hili. (alama 1)Question 10
- a) Mandhari ya onyesho hili ni mkahawani. Eleza manufaa matatu ya matumizi ya mandhari katika kazi yoyote ya fasihi…Question 11
- b) Eleza sifa mbili za Mabula zinazojitokeza wazi katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)Question 12