CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 11
a) Mandhari ya onyesho hili ni mkahawani. Eleza manufaa matatu ya matumizi ya mandhari katika kazi yoyote ya fasihi yaigizwayo. (alama 3)
From Test 85 — Kiswahili Paper 2 (KJSEA) · 3 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya Tamthilia ya 'Usife Moyo' (T. Arege) kisha ujibu maswali.
ONYESHO LA II
(Mabula na Temba wameketi mkahawani. Wanakunywa chai huku wanazungumza)
Mabula: (Akimwonyesha mavazi yaliyokunjana) Ona walivyonifanyia. Siwezi tena kupeleka nguo zangu kwa dobi. Hata huo umeme wa kunyoosha nguo siwezi kuumudu Temba. (Kwa hasira) Temba hebu niambie, kosa langu lilikuwa nini? Kusema kwamba pesa za umma zinakwenda mifukoni mwa watu binafsi ni makosa? Ni makosa kupigania watu wetu? Temba!
Temba: Si makosa. Ulifanya vizuri. Tatizo ni kwamba walioshika madaraka hawataki kuanikwa hadharani. Wanaogopa kumwaga unga wao.
Mabula: Temba, afadhali hata nisingesema. Wakubwa hawakusema kitu nilipofurushwa kazini. Hadi leo nimebaki kuhangaika badala ya kutuzwa. Waporaji wanasherehekea masaibu yangu.
Temba: Mabula, kama wanasherehekea ni kwa muda. Mambo yamebadilika kabisa. Mkurugenzi na naibu wake wameachishwa kazi. Wakubwa wamegundua kuna dosari mahali. Yaelekea habari sahihi zimewafikia.
Mabula: (Kwa upole) Kama kweli zimewafikia ninashukuru ila zimewafikia kuchelewa. Utu wangu umekwisha kuondoka. Heshima yangu haipo tena. Sina masilahi tena.
Temba: (Akimshika begani) Ninakuelewa ndugu yangu. Ninaielewa fika hali unayoipitia. Kumbuka kuwa ili mambo yanyooke lazima wachache wajitoe mhanga. Taifa linawategemea hao mashujaa wachache wa kweli. Wewe una bahati umekwisha kuingia miongoni mwa mashujaa wa kweli.
Mabula: Shujaa? Shujaa asiyeweza kukidhi mahitaji ya kimsingi? Hata imenifanya kuonja vileo isivyostahili Temba. Nimefikia kiwango cha kujiona mkosa kwa wapendwa wangu.
Temba: Mabula, itakuwa vizuri kuacha ulevi. Bado kuna matumaini ya kesho yenye faida na mafanikio. Usife Moyo.

Answer
Mandhari hukuza uhalisia wa tukio, hufafanua matukio na kueleza mazingira, humsaidia msomaji/mtazamaji kuelewa tukio, huongeza mvuto wa kazi, hujenga hisia, na hutambulisha wahusika.
Angalia jibu la mfano na vigezo vya alama hapo juu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- b) Eleza sifa mbili za Mabula zinazojitokeza wazi katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 2)Question 12
- c) Fafanua maudhui mawili makuu yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia. (alama 4)Question 13
- d) Eleza mojawapo ya mbinu za lugha (kama vile semi, tamathali za usemi) zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)Question 14
- a) Eleza nafsi nenewa (anayezungumziwa na mshairi) katika shairi hili. (alama 1)Question 15
- b) Eleza muundo wa shairi hili (kuzingatia mishororo, beti na vina). (alama 2)Question 16
- c) Dhamira kuu ya mshairi katika shairi hili ni gani? (alama 2)Question 17