CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 15
a) Eleza nafsi nenewa (anayezungumziwa na mshairi) katika shairi hili. (alama 1)
From Test 85 — Kiswahili Paper 2 (KJSEA) · 1 mark · Topic: Fasihi, Ushairi
Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha ujibu maswali.
Salamu nakutumia, ewe mtoto elewa,
Una kipawa sikia, na Mungu ulichopewa,
Katika hii dunia, kinafaa kutumiwa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Ni vyema ukifuatia, ukapata kukijua,
Kama ni cha kukimbia, chataka kuandaliwa,
Au watu kuimbia, wapate kufarijiwa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Yafaa kupalilia, na kukilea kipawa,
Ili uguse dunia, kwayo uliyojaliwa,
Lazima kunyunyizia, maji pamoja na dawa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Usiwe pundamilia, rangi mbili kuachiwa,
Huwezi kuwa mkia, na tena kichwa ukawa,
Kipi kinakuvutia, penye sahani na kawa?
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
(S. Kiponda)
Salamu nakutumia, ewe mtoto elewa,
Una kipawa sikia, na Mungu ulichopewa,
Katika hii dunia, kinafaa kutumiwa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Ni vyema ukifuatia, ukapata kukijua,
Kama ni cha kukimbia, chataka kuandaliwa,
Au watu kuimbia, wapate kufarijiwa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Yafaa kupalilia, na kukilea kipawa,
Ili uguse dunia, kwayo uliyojaliwa,
Lazima kunyunyizia, maji pamoja na dawa,
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
Usiwe pundamilia, rangi mbili kuachiwa,
Huwezi kuwa mkia, na tena kichwa ukawa,
Kipi kinakuvutia, penye sahani na kawa?
Kipawa cha kuishia, mtoto ulipatiwa.
(S. Kiponda)
a) Eleza nafsi nenewa (anayezungumziwa na mshairi) katika shairi hili. (alama 1)
Answer
Nafsi nenewa ni mtoto (kijana mwenye kipawa), anayehimizwa kutambua na kukuza kipawa chake.
Angalia jibu la mfano na vigezo vya alama hapo juu.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- b) Eleza muundo wa shairi hili (kuzingatia mishororo, beti na vina). (alama 2)Question 16
- c) Dhamira kuu ya mshairi katika shairi hili ni gani? (alama 2)Question 17
- ZOEZI I: INSHA (Alama 15) Swali la 1: Visa vya magonjwa yasiyoambukizwa vimekithiri katika mtaa wenu. Umealikwa…Question 1
- a) Taja wahusika wakuu wanne katika hadithi hii, mbali na Mzee Kobe. (alama 2)Question 2
- b) Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika hadithi hii. (alama 3)Question 3
- c) Taja methali mbili zilizotumiwa katika hadithi hii. (alama 2)Question 4