CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 21
Chagua jibu sahihi kukamilisha nafasi ya 21 iliyoachwa kwenye kifungu:
From Test 84 — Kiswahili Paper 1 (KJSEA) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Matamshi na Kusikiliza kwa Kina
Soma mazungumzo yafuatayo kati ya Pili na Tatu kisha ujibu maswali kuanzia la 21 hadi la 25.
(Ni asubuhi. Pili na Tatu wamekutana kipindi cha mapumziko nje ya darasa).
Tatu: (Akimnyoshea mkono). ___21___ ndugu?
Pili: Aheri mwenzangu. Habari za likizo fupi?
Tatu: (Akitabasamu) Njema rafiki yangu!
Pili: Mbona hukuwa shuleni juzi? Sikukuona kabisa.
Tatu: Tulienda kumzika mjomba Kitwana. Aliaga kutokana na maradhi ya kisukari.
Pili: (Kwa huzuni) Makiwa ndugu!
Tatu: Yameshapita.
Pili: Kwa kweli magonjwa yanayotokana na mienendo ya maisha yameongezeka sana.
Tatu: ___22___! Hata babu aliaga mwaka mmoja uliopita kutokana na saratani. Inasikitisha sana.
Pili: Je, ndugu yako amepata afueni baada ya kupigwa risasi mguuni alipokuwa akiandamana karibu na kituo cha polisi?
Tatu: Naam, ashatoka hospitalini na sasa anatumia kitimaguru.
Pili: Naamini kuwa siku moja tutapata haki. Unakumbuka namna walivyompiga risasi muuza maski?
Tatu: (Akitikisa kichwa) Naam, yaelekea kuwa askari aliyempiga risasi ametiwa mbaroni. Haki itatendeka?
Pili: Tungoje. Subira huvuta heri.
Tatu: Nakubaliana na wewe (wanakimbia kuelekea darasani).

21. Chagua jibu sahihi kukamilisha nafasi ya 21 iliyoachwa kwenye kifungu:
- AA. Masalkheri
- BB. Salaam aleikum
- CC. Shikamoo
- DD. Sabalkheri
Answer
D. D. Sabalkheri
Jibu sahihi: D. Sabalkheri.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu lenye neno ambalo Tatu angetumia katika nafasi ya 22 kuonyesha kukubaliana na Pili:Question 22
- Mbali na ugonjwa wa kisukari na saratani, ni ugonjwa gani mwingine ambao hutokana na mienendo ya maisha?Question 23
- Vipengele vifuatavyo vya kusikiliza na kuzungumza vimedhihirika katika mazungumzo haya ila:Question 24
- Ni kauli ipi ambayo ilitumiwa na Pili kufariji msiba wa Tatu?Question 25
- Kifungu kifuatacho kina nafasi ya 26 hadi 35. Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 26:Question 26
- Kifungu kifuatacho kina nafasi ya 26 hadi 35. Chagua jibu lifaalo zaidi kujaza nafasi ya 27:Question 27