CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 3
Mjomba alimpeleka Sali wapi? (Alama 1)
From Kiswahili — Extra-Activity Assessment 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
A. UFAHAMU (Alama 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Sali alikuwa mtoto mdogo alipokumbwa na masaibu makubwa. Ajali mbaya ilimpokonya wazazi wake na kumwacha yatima. Kwa muda mrefu, alihisi upweke mkubwa na maisha yake yalijaa mateso. Akiwa hana pa kwenda, alijikuta akizunguka mitaani bila mwelekeo, akiomba msaada kutoka kwa wapita njia.
Siku moja, alipokuwa ameketi kando ya barabara akiwa na njaa na uchovu, alikutana na mjomba wake aliyekuwa amemtafuta kwa muda mrefu. Mjomba huyo, aliyekuwa na huruma nyingi, alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake. Hapo, Sali alipata makazi mapya na upendo wa kifamilia alioukosa kwa muda mrefu.
Baada ya siku chache, mjomba alimwandikisha shule ya Kanyamedha. Hapo, Sali alipata marafiki wapya na maisha yake yakaanza kubadilika. Alisoma kwa bidii na kuonyesha juhudi kubwa darasani. Walimu wake walimpenda kwa kuwa alikuwa mnyenyekevu na mwenye bidii.
Siku moja, alipokuwa ametoka shuleni, alikutana na mjomba wake njiani. Wakati huo, Sali alikuwa akitabasamu, ishara kwamba alikuwa na furaha. Alimkimbilia mjomba wake, wakakumbatiana huku machozi ya furaha yakidondoka mashavuni mwao. Hatimaye, Sali alihisi kwamba alikuwa na maisha mapya yaliyojaa matumaini.
3. Mjomba alimpeleka Sali wapi? (Alama 1)
Answer
Nyumbani kwake (kwa mjomba).
"Mjomba huyo… alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake."
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ajali iliyompokonya Sali wazazi wake ilifanyika lini? (Alama 1)Question 4
- Sali alipelekwa shule gani? (Alama 1)Question 5
- Waliodondokwa na machozi ya furaha na kukumbatiana walikuwa nani na nani? (Alama 2)Question 6
- Ipe ufahamu uliosoma kichwa mwafaka. (Alama 2)Question 7
- B. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40) 1. Taja alama ifuatayo na utaje matumizi yake. (alama 1) •Question 8
- Jabez aliulizwa maana ya nomino na baada ya kujibu wanafunzi wote walimpigia makofi. Je, alijibu nomino ni nini?…Question 9