naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 3

Wanariadha wa Kenya wanajulikana kwa sababu ya

From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 – 6.
Mimi ni Mkenya mzalendo. Nchi ya Kenya imebarikiwa kwa mandhari ya kuvutia na watu wa mila mbalimbali. Mlima Kenya wenye kilele cha theluji, Mbuga ya Masai Mara yenye wanyama wa kila aina na fukwe safi za Pwani huvutia wageni kutoka sehemu zote za dunia. Wanariadha wetu mahiri wameiweka Kenya kwenye ramani ya dunia kwa kushinda mashindano makubwa ya riadha. Hili hunifanya kujivunia taifa letu.
Kenya ina rasilimali nyingi. Kuna misitu minene, mito yenye maanguko ya kuvutia kama Thika na Thomson’s Falls, na ardhi yenye rutuba kwa kilimo. Msimu wa masika huleta mvua nyingi inayochochea ukuaji wa mazao, huku kiangazi kikileta jua kali linalofaa kwa shughuli za kila siku. Ninajivunia kuwa sehemu ya nchi hii yenye hazina kubwa ya maliasili na watu wenye bidii. Je, nawe unajivunia kuwa Mkenya?

3. Wanariadha wa Kenya wanajulikana kwa sababu ya

  1. Auchezaji wa mpira wa miguu
  2. Bkushinda mashindano ya riadha duniani
  3. Ckuimba nyimbo za kitamaduni
  4. Dkuvumbua dawa mpya.

Answer

B. kushinda mashindano ya riadha duniani

Wameiweka Kenya kwenye ramani ya dunia.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test