CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 8
Mkutano wa viumbe uliitishwa kwa sababu viumbe walitaka
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 7 – 12.
Hapo zamani, Mungu aliumba viumbe vyote duniani, akawapa mazingira safi na ya kuvutia. Binadamu alipewa jukumu la kuwaongoza viumbe wengine kwa heshima na upendo. Hapo awali, walishirikiana bila matatizo, lakini baadaye binadamu alianza kujawa na tamaa. Alianza kutumia maji, madini, mito na wanyama kwa manufaa yake binafsi, jambo lililoleta hofu kwa viumbe wengine.
Mnyama mkubwa zaidi aliwaita viumbe wenzake. Walifanya mkutano na kukubaliana kumshtaki kwa Mungu yeyote atakayewaumiza wenzao. Binadamu hakuhudhuria mkutano huo kwa sababu aliwadharau. Baadaye alipokuwa akikata miti, viumbe waliamua kumkemea. Udongo ulionya binadamu, lakini alipokasirika, viumbe walianza kutoweka—miti ilizama, mito ikapotea, milima ikatetemeka na binadamu naye akamezwa. Huu ukawa mwanzo wa mauti na vifo.
8. Mkutano wa viumbe uliitishwa kwa sababu viumbe walitaka
- Akumchagua kiongozi mpya
- Bkusherehekea mazao mazuri
- Ckukomesha uovu wa binadamu
- Dkujifunza zaidi kutoka kwa binadamu
Answer
C. kukomesha uovu wa binadamu
Tamaa ya binadamu iliwatia hofu.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Ni mnyama wa aina gani aliyekuwa kiongozi wa mkutano?Question 9
- Kwa nini binadamu hakuhudhuria mkutano?Question 10
- Ni nani alionya binadamu dhidi ya vitendo vyake viovu?Question 11
- Binadamu alipokasirika, nini kilitokea?Question 12
- Tabia gani kuu iliyoonyeshwa na Adili?Question 13
- Ni nani alilalamika kwa kufichua siri?Question 14