CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2026 · Question 12
Binadamu alipokasirika, nini kilitokea?
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2026 (Set 8) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 7 – 12.
Hapo zamani, Mungu aliumba viumbe vyote duniani, akawapa mazingira safi na ya kuvutia. Binadamu alipewa jukumu la kuwaongoza viumbe wengine kwa heshima na upendo. Hapo awali, walishirikiana bila matatizo, lakini baadaye binadamu alianza kujawa na tamaa. Alianza kutumia maji, madini, mito na wanyama kwa manufaa yake binafsi, jambo lililoleta hofu kwa viumbe wengine.
Mnyama mkubwa zaidi aliwaita viumbe wenzake. Walifanya mkutano na kukubaliana kumshtaki kwa Mungu yeyote atakayewaumiza wenzao. Binadamu hakuhudhuria mkutano huo kwa sababu aliwadharau. Baadaye alipokuwa akikata miti, viumbe waliamua kumkemea. Udongo ulionya binadamu, lakini alipokasirika, viumbe walianza kutoweka—miti ilizama, mito ikapotea, milima ikatetemeka na binadamu naye akamezwa. Huu ukawa mwanzo wa mauti na vifo.
12. Binadamu alipokasirika, nini kilitokea?
- AAliomba msamaha kwa viumbe wote.
- BMiti, wanyama, mito na milima vilianza kutoweka.
- CAliwakamata wanyama wote.
- DAlijenga nyumba kubwa ya kuishi.
Answer
B. Miti, wanyama, mito na milima vilianza kutoweka.
Viumbe walianza kutoweka.