CBC Grade 8 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 8
g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa taarifa. i. Mhimili
From Kiswahili — End Term One Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuata.
Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na “wanyama wala watu.” Katika wimbo “Babylon System” (yaani mfumo wa kibepari), Marley alisema kuwa utamaduni huo ndio mzawa wa matatizo yote ya kiutawala ambayo yalikuwa yakiyakumba mataifa ya Weusi katika karne ya 20, wakati nchi zao zilikuwa zikitawaliwa na nchi za mataifa ya Ulaya.
Kwa mantiki hiyo, pengine Marley alikuwa na maono kuwa Afrika haingejikomboa kutoka kwa utumwa wa Kizungu, ikiwa ingeendelea kuziabudu na kuzishadidia tamaduni za Kimagharibi.
Utabiri huo nauoanisha na yanayoendelea nchini, ambapo serikali ya Jubilee imeonekana kushindwa kabisa kuikabili saratani ya ufisadi, ambayo inahatarisha kuliangamiza taifa hili lenye uchumi dhalili.
Donda hili linazidi kuyatandaza mabawa yake kutoka, tisho kuu likiwa ni uvamizi wa taasisi “takatifu” ambazo tunazitegemea kulikabili donda hilo.
Ni nani tutategemea kukabiliana na rushwa ikiwa taasisi kama Bunge, Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) kati ya zingine muhimu zimepakwa tope na saratani hiyo?
Kimsingi yote tunayopitia ni matunda ya uasi wa tamaduni za Kiafrika na uegemezi wa mifumo ya Kizungu kama mihimili ya jamii na nchi zetu.
Ndoto za watetezi wa Uafrika na nafasi ya Weusi kama marehemu Malcolm X na Martin Luther King, zilikuwa ni kuona kuwa wameungana kabisa kukabiliana na matatizo yaliyowakabili bila kuzingatia mazingira waliyokuwemo.
Pindi tu baada ya mataifa mengi ya Kiafrika kujinyakulia uhuru wao katika miaka ya hamsini na sitini, viongozi wakuu walioziongoza nchi hizo kama Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kati ya wengine walianza harakati za kuliunganisha bara hili na kubuni Muungano wa Nchi za Kiafrika (OAU) japo ndoto hiyo haikufikia.
Kwa msingi huo, mhimili mkuu wa kiutawala ungekuwa ni mfumo wa kisosholisti, ambao ungekuwa nguzo kuu ya kuyaunganisha mataifa hayo.
Hata hivyo, migawanyiko mikubwa ilianza kushuhudiwa, huku baadhi ya mataifa yakianza kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutaasisika kwa maovu yote tunayoshuhudia sasa: ufisadi na tamaa ya kuogofya kutoka kwa viongozi wetu.
g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa taarifa.
i. Mhimili
Answer
Nguzo / msingi
"mihimili ya jamii", "mhimili mkuu wa kiutawala".
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- MUHTASARI a) Fupisha aya mbili za kwanza. (maneno 65-70) (alama 8, utiririko 2)Question 10
- b) Eleza ni vipi ukiukaji wa haki za watoto unaweza kuepukwa. (maneno 30-35) (alama 4, utiririko 1)Question 11
- MATUMIZI YA LUGHA / SARUFI a) Eleza sifa bainifu za sauti /j/. (alama 2)Question 12
- b) Fafanua maana ya shadda. (alama 2)Question 13
- c) Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii. AlivyolikimbiliaQuestion 14
- d) Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii. Nyanya ametengenezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.Question 15